Diamond Platnumz aondoka leo (March 30) kwenda Nigeria kufanya video mpya - Picha

diamond lagos trip-1
Diamond akiwa na Bab Tale tayari kwa safari yao
Wiki iliyopita Diamond Platnumz alisema anatarajia kusafiri kwenda nchini Nigeria (March 30) kwaajili ya kufanya video ya wimbo wake mpya aliofanya collabo na mastaa wa huko.

Usiku wa kuamkia leo Platnumz amepost picha Instagram akiwa ameongozana na meneja wake Bab Tale wa Tip Top Connection, wakiwa uwanja wa ndege JNIA tayari kwa safari yao ya Lagos.
diamond lagos trip-2 Wema hakukosa kumsindikiza kipenzi chake uwanja wa ndege
Hivi karibuni hit maker huyo wa ‘Number 1’ alisema mbali na kushoot video, kitu kingine anachoenda kukifanya Nigeria ni pamoja na kufanya collabo zaidi na wasanii wa huko kwa lengo la kuliteka soko la Afrika kwa ujumla.

Post a Comment

Previous Post Next Post