Jose Chameleone amenyang’anywa gari yake aina ya Escalade na
maofisa wa URA baada ya mamlaka hiyo kudai kwamba msanii huyo ameshindwa
kulipa kodi yenye thamani ya shilingi milioni saba ya Uganda.
Muda mchache kabla ya kuanza kwa onyesho kubwa la Tubonge la msanii
huyo, maofisa wa URA waliikamata gari yake hiyo ya kifahari.

Kibali toka URA
Kwa mujibu wa mtandao wa Redpapper wa nchini Uganda,msanii huyo
alijaribu kuwakatalia wasikuchukue gari lake akidai atakufa na mtu
atakayeichukua lakini kauli hiyo haikufua dafu kwa mamlaka hiyo. “Hii ni
gari yangu binafsi na nina haki yake, mtu yeyote akigusa Escalade
yangu, nami tufe pamoja naye,” alidai Chameleone.
Hata hivyo Chameleone alidai kuwa hana tatizo lolote kulipa kodi
lakini mamlaka hiyo haikutolea vigezo walivyotumia kupata jumla ya
shilingi milioni 7 za Uganda ambazo ndizo pesa wanazomdai.
Source:Redpapper
إرسال تعليق