Ulishawahi
kujiuliza kwanini video ya Shakira na Rihanna haikuwa na model yoyote
wa kiume? Inawezekana hili likawa moja ya jibu: Gerard Pique hataki
mchumba na mama wa mtoto wake Shakira afanye video akiwa
na mwanaume mwingine.
Kwa mujibu mahojiano aliyoyafanya na
jarida la Billboard Magazine, Shakira amesema haruhusiwi kufanya video
na wanaume wengine, hiyo ni amri ya mchumba wake Pique ambaye ni
mwanasoka wa FC Barcelona.
“Pique hataki nifanye video na wanaume, ndio maana ikabidi video yetu iwe ya wanawake tu.”
Shakira aliendelea, “Hili suala
halina mjadala tena, mie nimekubaliana nalo na nimependa, anaonyesha
kwamba anapenda kulinda mali yake na ananithamini, kiasi kwamba hataki
mwanaume mwingine aushike au kutazama mwili wangu kama alivyofanya
Rihanna,” alisema Shakira huku akicheka.
إرسال تعليق