
Serikali ya Malaysia imeomba
kupewa radar zaidi pamoja na data ya satelite kutoka kwa mataifa mengi
huku ikijitahidi kutafuta eneo la ndege ya kampuni ya Malaysia Airline
iliopotea zaidi ya wiki moja iliopita.
Waziri wa uchukuzi nchini Malaysia Hishamuddin Hussein amesema kuwa takriban mataifa 25 yanashiriki katika kuitafuta ndege hiyo.Kwa siku ya pili mfululizo maafisa wa polisi wamezuru katika nyumba ya nahodha mkuu Zharie Shah huku uchunguzi ukiendelea kuwaangazia abiria wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo.
Naye ndugu mmoja ya mwathiriwa wa ndege hiyo amesema kuwa hatakwenda nyumbani hadi pale atakapopata majibu kamili kuhusiana na ndege hiyo.
Kwa sasa Malaysia inaangazia njia mbili ambazo huenda ndege hiyo ilielekea, nazo ni ukanda wa kazkazini na ule wa kusini.
إرسال تعليق