MB Dog: Msanii bila menejimenti ni sawa na kazi bure

Mb.DogMsanii wa muziki aliyefanya vizuri kipindi cha nyumba MB Dog amesema msanii bila kuwa na management ni sawa na kufanya kazi bila malengo.
Ameiambia Bongo5 kuwa amehangaika kufanya muziki peke yake bila mafanikio ndio maana aliamua kurejea Tip Top Connection.
“Tip Top nilitoka na ndio kitu ambacho kilinirudisha nyuma sana,” amesema. “Pale nilikuwa nafanyiwa kila kitu, nilikuwa narekodi tu kazi yangu vitu vingine vyote wanafanya wao so baada ya kutoka na kujisimamia mwenyewe nikaanza kuyumba na kuhangaika huku na kule. Kwahiyo kitu ambacho nimegundua msanii bila management nzuri huwezi fika mbali asikwambie mtu. Msanii anahitaji kuongozwa, kushauriwa na mambo mengine. Sasa hivi nipo Tip Top tumeingia makubaliano mapya ya kazi ndio maana nashukuru Mungu ngoma yetu mpya ‘Umenuna’ inasonga kidogo kidogo mpaka kieleweke.”

Post a Comment

Previous Post Next Post