
Mrembo
Sarah Paul aliposhiriki furaha yake ya siku ya kuzaliwa na watoto wa
kituo cha TZ 820 FPTC NG'AMBO STUDENT CENTER - Kilichopo Tabora.

Kila mmoja alipata nafasi ya kufurahia keki iliyoandaliwa maalumu kwa watoto hao.



Baadhi ya vitu alivyowaandalia watoto hao na kuvikabidhi kwenye shirika hilo.

Sarah
Paul, mshindi wa shindano la urembo la Redds Miss Tabora 2012, ambaye
pia mwaka jana alishiriki katika shindano hilo hadi kufikia fainali za
Miss Tanzania.
****
Leo
katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa amefanikiwa kuwatembelea
watoto wanakusanywa na kanisa la FPCT NG'AMBO wanaopewa msaada na
Shirika la Compassion International Tanzania na kuwasaidia watoto
wanaoishi katika mazingira magumu. Watoto hawa wanakusanywa kwa lengo la
kuwatoa na kuwakomboa umaskini wa kiuchumi, kijamii, kimwili na kiroho
na kuwawezesha waje wawe watu wazima wanaojua wajibu wao na kujitegemea.



Mrembo huyo akiongea na watoto




Richard,
mmoja wa wanafunzi wa chuo kikuu kishiriki cha SAUT (SAUT-TABORA)
AMUCTA anayesomea Mahusiano ya Umma na Masoko akiongea na watoto.

Miss Pauline (Mshindi namba 3 wa chuo cha Utumishi wa Umma-Tabora) akiongea na watoto.



Sarah akikata keki na watoto.





Suleiman H. Halletu (Mkurugenzi wa kituo) akishukuru baada ya kupokea zawadi za mrembo Sarah kwaajili ya watoto.


Team
nzima iliyomsindikiza mrembo katika hafla hiyo fupi. Kutoka kulia ni
Marry, Richard, Miss Zennah (Miss Singida 2012/13), Miss Pauline, Miss
Sarah (MissTabora2012), Miss Lilian (Mshindi No2 TPSC 2013), na Annah
Henry (Afisa Ugani)
إرسال تعليق