Muimbaji wa Kenya, Mwanaisha Abdallah Mohamed maarufu kama Nyota
Ndogo, ameungana na wanawake wa Mombasa kufanya maandamano ya kupinga
udhalilishaji dhidi yao unaofanywa na rapper, Colonel Mustafa ikiwa ni
pamoja na kupost kwenye mitandao picha za wanawake wakiwa mtupu.
“Mimi naona kama Mustafa anatusi muziki, anatusi wanawake, anatusi
mama yake. Kwahiyo Mustafa aombe msamaha kwa wanawake,” alisema Nyota
Ndogo.
Mustafa anadaiwa kumtumia Huddah Monroe kujipatia umaarufu baada ya
kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa wana uhusiano wa kimapenzi.
Baadaye Huddah alikanusha na kusema yote yalipangwa.
Post a Comment