Producer wa muziki wa anayejulikana kwa jina la Mswaki Kutoka
studio ya Black Curtains amesema wiki hii anatarajia kuelekea mjini
Morogoro kwa Mama Albert Mangwea kuchukua kibali cha kufanya style ya wa
mwanae kibiashara.
Akizungumza na 255 ya XXL ya Clouds FM, jana Mswaki, amesema kuwa
hataki kuwa na maswali mengi juu ya kutumia style hiyo ndio maana
ameamua kwenda kwa Mama Mangwea.
“Kwa upande mwingine kama mzazi anaweza akaona sio sahihi,sijui
labda, so sitaki niwe na maswali mengi sana nikaona kwamba ninaweza
nikaenda Morogoro kuongea na mama yake ni msikie yeye anasemaje,
nikamsikilizishe nyimbo na nini,” alisema producer huyo. “Mimi ninavyo
hisi hiki kitu kinaweza kuwa na faida gani kwa muziki wa Albert na yeye
aone kama ataona sawa aseme kama ni sawa ninaweza nikaendelea kuifanya
au kama sio sawa. So kama akisema ni sawa mimi nitajua naipush kwa
ukubwa gani kunzia ila nataka kwanza nimsikie yeye mwenyewe binafsi.
Familia ita benefit percent nitagawa percent sijajua mpaka sasa hivi ni
percent ngapi? Iwe 50,50, mimi nitagenga some of my time nitapanga
ratiba yangu vizuri tu ya kazi zangu zisiingiliane kwasasabu huko
itabidi ni act kama msanii sasa unajua kuna ma interview, shows kuna
nini ,na upande mwingine mimi ni music producer kwahiyo itabidi nipange
ratiba yangu sawa niko radhi kuipanga ratiba yangu kihivyo ili tu hiki
ninachokifanya kifike pale ambapo mimi naona ni sawa ni sehemu sahihi.”
Post a Comment