
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mjumbe Maalum wa Rais wa
Afrika Kusini Mhe. Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya
Nje wa nchi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam leo.

Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika
Kusini Mhe. Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa
nvhi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam leo. (Picha na Ikulu).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumapili, Machi 16, 2014, amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais
Jacob Zuma wa Afrika Kusini.
Ujumbe
huo wa Rais Zuma umewasilishwa kwa Rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya
Nje wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Maite Nkoana-Mashabane wakati mama huyo
alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu, Dar Es
Salaam.
Mara
baada ya kuwasilisha ujumbe huo, viongozi hao wamejadili masuala
yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini na masuala ya
kikanda ambako nchi zote mbili ni wanachama wa Jumuia ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC).
Mheshimiwa Nkoana-Mashabane amendoka nchini mara baada ya kuwasilisha ujumbe huo kwa Rais Kikwete.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
16 Machi,2013
إرسال تعليق