Robin Van Persie nje wiki 6 – hizi ndio mechi atazokosa

.article-2586288-1C6E285700000578-240_634x399Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Robin van Persie ameripotiwa kwamba amepata majeruhi ya goti baada ya kuumia katika mchezo wa raundi ya pili wa hatua ya 16 ya ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Olympiakos uliopigwa katika dimba la Old Trafford, jumatano wiki hii.

Van Persie ambaye alifunga hat trick iliyoipeleka Man United hatua ya robo fainali alitolewa nje na machela katika mchezo huo katika dakika za mwisho za huo, na leo hii baada ya kufanyiwa vipimo kiundani imegundulika amepata majeruhi yatakayomuweka nje kwa muda wa wiki 4-6.

Kwa maana hiyo mdachi huyo atazikosa mechi zifuatazo
Mar 23: West Ham (A) Mar 25: Man City (H) Mar 29: Aston Villa (H) Apr 1: Bayern Munich (H) Apr 5: Newcastle (A) Apr 9: Bayern Munich (A) Apr 20: Everton (A) Apr 26: Norwich (H.

Post a Comment

Previous Post Next Post