Kamera
za usalama zikimwonyesha rubani wa ndege ya Malaysia aina ya Boeing
777, Zaharie Ahmed Shah, kwenye uwanja wa Kuala Lumpur.
Michoro inayoonyesha njia ambayo ndege hiyo huenda ilipitia kwenda kusikojulikana.
Mwanafunzi,
Firman Siregar, akiwa na wazazi wake, ni mmoja wa abiria 239 waliokuwa
katika ndege hiyo yenye orodha ya safari namba Flight MH370.
Rubani Zaharie Ahmad Shah.
Nyendo za ndege hizo zinavyokisiwa na wataalam.
Mwandishi wa habari akichukua picha nyumba ya rubani Fariq Abdul Hamid eneo la Shah Alam, karibu na Kuala Lumpur.
Maafisa
nchini Malaysia wamefichua kwamba wanadhani rubani mwenza katika ndege
ya Malaysia iliyotoweka ndiye aliyezungumza maneno ya mwisho kabla ndege
hiyo kutoweka.
Maneno
hayo bado hayajabainika lakini yanasikika kama -- all right, au
goodnight -- ''Kila kitu ki shwari au muwe na usiku mwema'', kabla ya
vifaa vinavyowezesha ndege kutambulika katika mtambo wa rader kuzimwa.
Wachunguzi wanaangalia uwezekano kuwa huenda marubani walihusika katika tukio hilo.
Juhudi
za kimatifa za kutafuta ndege hiyo pia zinazingatia njia mbili ambazo
huenda ndege hiyo ilifuata kwani inaaminika kuwa ilipaa kwa saa kadhaa
baada ya mitambo ya mawasiliano kuzimwa.
CHANZO: PICHA DAILYMAIL / HABARI BBC SWAHILI
Post a Comment