
Mkurugenzi
wa Masoko na Mauzo wa Serena Hotel Bw. Seraphin Lusala
(katikati)akiangalia moja ya aina ya taa zinazotumia umeme mdogo wakati
wa hafla ya Saa za Dunia (Earth Hour) jana jijini Dar es Salaam. Earth
Hour ni harakati zinazofanyika kila mwaka duniani kote zikiwa na lengo
mahususi la kutunza mazingira na nishati , katika hafla hiyo ambayo
ufanyika kila Jumamosi ya mwisho ya mwezi machi taa uzimwa kwa muda wa
saa moja kuannzia saa 2:30 usiku hadi saa 3:300.kulia ni Afisa Mauzo wa
kampuni ya Smart Sense Venu Sree na kushoto ni Mkurugenzi wa Smart
Sense Bw. Kalpesh Babaria.

Mkurugenzi
wa Smart Sense Bw. Kalpesh Babaria akitoa maelezo kuhusu taa aina ya
LED ambazo zimebuniwa mahususi kupunguza matumizi makubwa ya nishati ya
umeme na uharibifu wa mazingira,wakati wa hafla ijulikanayo kama Earth
Hour ambayo lengo lake ni kuhifadhi na kutunza mazingira.

Kutoka
kushoto ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania,
Bi. Neema Rose Singo akisoma maelekezo kuhusu taa za LED wakati wa
hafla ya Earth Hour iliyofanyika Serena Hotel jana jijini Dar es Salaam,
wanaofuatia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Dar es Salaam Serena
Hotel Bw. Seraphin Lusala, Afisa Mauzo wa kampuni ya Smart Sense Venu
Sree na Mkurugenzi wa Smart Sense Bw. Kalpesh Babaria.

Mkuu
wa Masoko wa Exim Bank Tanzania Bw. Noel Tuga akipata maelekezo kutoka
kwa Afisa Mauzo wa kampuni ya Smart Sense Venu Sree kuhusu matumizi ya
taa za kisasa aina ya LED ambazo zinatumia nishati kidogo.

Mkurugenzi
wa Masoko na Mauzo wa Serena Hotel Bw. Seraphin Lusala (mwenye suti
nyeusi) akifurahi pamoja na wageni na wafanyakazi wenzake baada ya
kuadhimisha Saa ya Dunia (Earth Hour) jana jijini Dar es Salaam. Earth
Hour ni harakati zinazofanyika kila mwaka duniani kote zikiwa na lengo
mahususi la kutunza mazingira na nishati , katika hafla hiyo ambayo
ufanyika kila Jumamosi ya mwisho ya mwezi machi taa uzimwa kwa muda wa
saa moja kuanznia saa 2:30 usiku hadi saa 3:30 usiku.(Picha na Frank
Shija).
إرسال تعليق