
Baadhi ya Wanafunzi wa Skuli ya Kitope
waliohudhuria hafla ya kupatiwa vikalio vya skuli za Donge na Kitope
iliyofanyika katika Skuli ya Sekondari ya Kitope.

Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif
Ali Iddi akipokea Madeski 50 kwa ajili ya skuli ya Sekondari ya Kitope
kutoka kwa Meneja wa Tawi la Benki ya NMB Bwana Bakari Khamis Mohd.

kwa Meneja wa Tawi la Benki ya NMB
Bwana Bakari Khamis Mohd akimkabidhi madeski 50 Mbunge wa Jimbo la Donge
Mh. Sadifa Juma Khamis kwa ajili ya Skuli ya Sekondario ya Doonge.

Balozi Seif akiwa katika picha ya
pamoja na Uongozi wa Benki ya NMB mara baada ya hafla ya makabidhiano ya
madeski kwa ajili ya skuli za Donge na Kitope.
Kushoto ya Balozi ni Mbunge wa Jimbo la Donge Mh. Sadifa Juma mKhamis na Mke wa Balozi Seif Mama Asha Suleiman Iddi.
Kulia
ya Balozi ni Meneja wa NMB Tawi la Zanzibar Bwana Bakari Khamis Moha na
Mwenyekiti wa Skuli ya Kitope Sekondari Nd. Ali Mussa.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Benki
ya kuhudumia Wananchi wa Kawaida Nchini { NMB } imekabidhi mchango wa
Vikalio 100 kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu katika Skuli za
Sekondari za Donge na Kitope zilizomo ndani ya Wilaya ya Kasakazini “ B “
Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Msaada
huo wa Vikalio wenye gharama ya shilingi za Kitanzania Milioni Kumi
utasaidia kupunguza uhaba wa madeski kwa Skuli hizo za Donge na Kitope
ambapo kila Skuli imefanikiwa kupata madeski 50.
Meneja
wa Tawi la NBC Zanzibar Bwana Bakari Khamis Moh’d alikabidhi msaada huo
kwa Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Mbunge wa
Jimbo la Donge Mh. Sadifa Juma Khamis hafla iliyofanyika hapo katika
skuli ya Sekondari Kitope.
Meneja
huyo wa Tawi la Benki ya NMB Bwana Bakari aliiomba Jamii kuendelea
kuiunga mkono Benki hiyo ili kusaidia kuipa nguvu za kiutendaji
itakaoongeza kasi ya kusaidia harakati za Kijamii Nchini.
Alisema
Benki hiyo tokea kuasisiwa kwake mnamo mwaka 1997 imekuwa ikijitahidi
kuunga mkono maendeleo ya Wananchi hasa katika miradi iliyomo ndani ya
Sekta ya Elimu.
Akitoa
shukrani zake mara baada ya kupokea msaada huo wa vikalio Mbunge wa
Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi ameziomba Benki nyengine Nchini kuiga mfano wa Benki ya
NMB katika kusaidia maendeleo ya Wananchi.
Balozi
Seif alisema taasisi za Kifedha ndani na nje ya nchi zimekuwa na mfumo
maalum unaosaidia kuunga mkono juhudi za jamii katika maeneo tofauti ya
kiuchumi na ustawi wa jamii.
Alisema Wananchi hawanabudi kushirikiana na kuzipa nguvu taasisi hiyo ili ziweze kutekeleza malengo zilizojipangia.
“
Ukweli halisi NMB ni Benki ya wanyonge. Ni Benki yetu inayolenga
kuhudumia wananachi wa kipato cha chini. Huyu ndie rafiki yetu na
tunapaswa kumuunga mkono “. Alisema Balozi Seif.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Donge Mh. Sadifa Juma Khamis alisema Benki ya NMB
imeonyesha umahiri mkubwa katika kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya CCM ya
mwaka 2010 ambayo imejipangia kuimarisha Sekta ya Elimu iliyo muhimili
pekee wa maendeleo ya kiuchumi kwa Taifa lolote Duniani.
Akisoma
risala ya Walimu na wazazi wa Skuli za Donge na Kitope Mwalimu Mkuu wa
Skuli ya Sekondari ya Kitope Mwalimu Suleiman Juma Makame ameupongeza
Uongozi wa Benki hiyo pamoja na ule wa Jimbo la Kitope kwa juhudi zao
zilizojikita zaidi katika kuimarisha Sekta ya Elimu.
Hata
Hivyo Mwalimu Suleiman alisema zipo changa moto zinazoendelea kuzikabili
skuli hiyo akatolea mfano wa Skuli yake ya Kitope inayokabiliwa na
uhaba wa Vifaa vya Maabara pamoja na uwezekwaji wa jengo moja la Skuli
hiyo.
Akitoa
salamu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Afisa Elimu wa
Wilaya ya Kaskazini “B “ Mwalimu Ussi Machano alieleza kwamba mchango wa
Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif katika Sekta ya Elimu umekuwa
mfano wa kuigwa na Viongozi wengine hapa Nchini.
Mwalimu
Ussi Machano alisema kwamba mchango huo kwa kiasi kikubwa umeipunguzia
mzigo mkubwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika ukamilishaji
wa Majengo mbali mbali ya Skuli yanayoanzishwa na wananchi wenyewe kwa
mpango wa kujitolea.
Huu ni mkupuo wa Pili kwa Benki hiyo ya NMB kusaidia vikalio kwa Skuli za Donge na Kitope.
Post a Comment