
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 28.03.2014
Mnamo tarehe
28.03.2014 majira ya saa 02:10 usiku huko Gulwe katika Wilaya ya Mpwapwa
kulitokea ajali ya treni ya mizigo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda
Kigoma baada ya kusombwa na mkondo wa maji ya mvua zinazoendelea kunyesha.
Kutokana na wingi na nguvu ya maji hayo ilifanya kichwa cha treni hiyo
kutumbukia kwenye mto Mimo.
VIFO:
Ajali hiyo hadi
hivi sasa imesababisha vifo vya watu wawili ambao wamefahamika kwa majina
yafuatayo:-
1. Felix s/o Kalonga
2. Ismail @ Suma
MAJERUHI:
Waliojeruhiwa ni
kama ifuatavyo:-
1. Hassan
s/o Kitambo, Mhehe, Miaka 89, Mkazi wa Kidete – Amelazwa katika Hospitali ya
Mpwapwa.
2. Reuben
Ngasongwa, Miaka 43 – Amehamishwa kutoka Hospitali ya Wilaya Mpwapwa kupelekwa
Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
3.Michael Lupatu,
Mbondei, Miaka 52 – Amehamishwa kutoka Hospitali ya Mpwapwa kwenda Hospitali ya
Mkoa wa Morogoro.
4. Ramadhan
Kanenda, Miaka 34, Mnyamwezi – Amelazwa Mpwapwa Hospitali.
5.Mohamed Salum,
Miaka 25, - Alitibiwa na kuruhusiwa
6. E.2699
CPL Mfaume – Ametibiwa na kuruhusiwa.
7.E.3295 CPL
Respis – Bado amelazwa Mpwapwa Hospitali.
Bado jitihada za
kuwatafuta watu wengine wanne ambao hawajulikani walipo zinaendela.
إرسال تعليق