
Chama cha upinzani MSD chake Alexis Sinduhije kimezuiwa kuendelea na shughuli zake kwa miezi minne
Umoja wa mataifa na Muungano wa
Ulaya zimeelezea wasiwasi kuhusu mvutano wa kisiasa unaozidi kutokota
kati ya serikali na vyama vya upinzani nchini Burundi.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon,
amelaani hali ya kisiasa nchini humo,akisema kuwa serikali inakandamiza
uhuru wa kisiasa, uhuru wa kuongea na watu kukutana.Kwa upande wake afisaa mkuu wa maswala ya kidiplomasia katika Tume ya Ulaya, Catherine Ashton, ametaka pande zote za kisiasa kushauriana
Agizo hili linatokana na ghasia za kisiasa kati ya wanaharakati wa upinzani na polisi mapema mwezi huu.
Wiki jana mahakama nchini humo ilimchukulia hatua kiongozi wa chama cha upinzani (Movement for Solidarity and Development party) ambaye pia ni mwandishi habari wa zamani, Alexis Sinduhije na wanaharakati wengine 71 kwa madai ya njama ya mapinduzi.
Hii ni baada ya maandamano yao salama ya Tarehe 8 mwezi huu kugeuka na kua vurugu kati ya wapinzani hao na polisi.
Huku hayo yakiarifiwa serikali ya Burundi imechukua hatua ya kusitisha shughuli zote za chama cha upinzani cha MSD kwa kipindi cha miezi minne baada ya kukishutumu kwa kuzua vurugu.
Chama hicho kimekanusha kusababisha vurugu zozote.
Post a Comment