Nahodha wa Liverpool,Steven Gerrard
anaamini kuwa ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Manchester United kwenye
uwanja wa Old Trafford umeleta matumaini zaidi ya kushinda taji la ligi
kuu ya Uingereza.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 alifunga
penati mbili na kukosa ya tatu wakati Nemanja Vidic alipotolewa nje
kabla ya Luis Suarez kufunga kwenye dakika sita kabla ya mpira kuisha.
Ushindi huo ulifanya kikosi hicho cha Brendan
Rodgers kupanda mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakiwa nyuma
ya Chelsea kwa pointi nne lakini wakiwa na mchezo mmoja mkononi huku
ratiba ikionesha michezo dhidi ya Manchester City na vinara hao bado
itapigwa Anfield.
Liverpool hawajapoteza mchezo wowote wa ligi
tangu kuingia kwa mwaka 2014 wakishinda michezo nane kati ya 10 na
wanamatumaini makubwa sana ya kutwaa taji la kwanza la ligi kuu ya
Uingereza katika kipindi cha miaka 24.

Katika hatua kama hii msimu uliopita,Man United walikuwa pointi 29
mbele ya Liverpool.Na sasa wapo mbele kwa pointi 14 dhidi ya mashetani
wekundu hao na Gerrard anaamini hii inatokana na jinsi walivyojiandaa
vizuri na kujituma kwa nguvu zaidi.
Nyota huyo alisisitiza kuwa,”Nafikiri tumeonyesha leo(Jumapili) kuwa
sisi ni wapinzani wakubwa na tunaenda kupambana mpaka tuone mwisho
wake.”
Na akaongeza kuwa amecheza katika dimba la Old Trafford kwa miaka
mingi na ni timu bora huku akikiri kuwa sehemu hiyo ni ngumu zaidi
kucheza vizuri na kumudu mchezo mwanzo mpaka mwsiho na kuibuka na
ushindi.

Pia akaongelea kuhusu penati zake na kusema kuwa,”Nilikuwa imara na
mwenye kujiamini sana lakini katika penati ya tatu sikuhisi kama ntakosa
ila penati ya pili niliifurahia zaidi.”

Gerrard alidai kuwa wanachoangalia sasa ni kujitahidi kushinda mchezo
unaofuatia dhidi ya Cardiff City kama walivofanya kwa Man United na
baadae kufanya hivyo tena dhidi ya Sunderland na michezo mingine ili
waweze kuwa katika hali nzuri zaidi katika mbio zao za Ubingwa.

Licha ya nahodha huyo wa timu ya Taifa ya England kipindi cha nyuma
kuwahi kukataa kabisa kuhusu Liverpool kuwania taji la ligi huku akisema
wanatazamia kupata tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa
barani Ulaya alithibitisha kuwa kwasasa wana uwezo wa kufanya hivyo na
watajitahidi kuendelea kufanya vizuri.
Post a Comment