Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke,
Engelbert Kiondo, alisema jana kuwa Kijazi alijiua juzi saa 11:15 jioni
katika maeneo ya Mtoni Kijichi, Wilaya ya Temeke.
Alisema Kijazi alikutwa amejinyonga kwa kutumia kitambaa cha nguo alichokitundika kwenye kenchi ya choo ya nyumba anayoishi.
Ujumbe
uliokutwa katika eneo hilo ulisomeka: “Hajahusika mtu yeyote kuhusu
hili, nimemmiss Mama John wangu, nizikwe Dar es Salaam na Mchungaji
Haule naomba ujumbe huu uheshimiwe.”
Kwa mujibu wa Kamanda Kiondo,
uchunguzi wa awali umebaini kuwa Mama John alifariki mwaka 2012 baada ya
kuugua malaria na tangu wakati huo Kijazi alikuwa akijaribu kujiua na
kuokolewa na ndugu zake. Maiti amehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke.
Katika
tukio jingine, Kamanda Kiondo alisema, Mwendesha Pikipiki, Said Jongo
(32) amekufa papo hapo baada ya kugongwa kwa nyuma na gari aina ya
Toyota Coaster lenye namba T412 ATJ.
Ajali hiyo ilitokea juzi saa
12:00 jioni katika Barabara ya Chamazi eneo la Charambe Magengeni,
ambapo gari hilo likiendeshwa na mtu asiyefahamika akitoka Mabagala
Rangi Tatu kwenda Chamazi, liligonga kwa nyuma pikipiki yenye namba
T281 CKY aina ya Fekon, iliyokuwa ikiendeshwa na Jongo.
Mwili wa
Jongo umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke na dereva wa gari hilo
aliyekimbia baada ya ajali bado anatafutwa, gari liko katika Kituo cha
Polisi Mbagala.
Katika tukio la tatu, mkazi wa Majohe aliyetambuliwa
kwa jina la Erasmus Marshal (52), amekutwa amekufa chumbani kwake huku
mwili ukiwa umeanza kuharibika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala,
Marietha Minangi, alisema mwili wa Minangi ulikutwa juzi saa 7:00 mchana
huko Majohe Kichangani ukiwa umekaa kitandani huku umefunikwa shuka na
mezani kwake kulikutwa mabaki ya chakula aina ya utumbo na soda ya Azam
Malta.
Uchunguzi wa awali kwa mujibu wa Kamanda Minangi, umeonesha
kuwa enzi za uhai wake alikuwa akiishi peke yake kwenye nyumba hiyo na
mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa
uchunguzi zaidi.
إرسال تعليق