Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi la Magereza, Deonice 
Chamulesile akiwaongoza Mamia ya Waombolezaji katika kutoa heshima za 
mwisho kwa Marehemu Sajini wa Magereza, Peter Shelukindo aliyefariki kwa
 ajali ya gari Aprili 22, 2014 majira ya saa Saba mchana wakati 
akisindikiza Mahabusu kutoka Mahakama ya Mwanzo Kimanzichana Wilayani 
Mkuranga, Mkoa wa Pwani. Katika ajali hiyo pia walikufa Mahabusu wanne 
waliokuwa wanatoka kusikiliza kesi zao.
 
 
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Magereza wakiaga mwili wa Marehemu 
Sajini wa Magereza, Peter Shelukindo katika Kambi ya Chuo cha Maafisa 
Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam  Aprili 24, 2014.
 
 
Mke wa Marehemuakisaidiwa na mmoja wa Waombolezaji kumuaga Mme wake aliyekufa kwa ajali ya gari.
 
 
Baadhi ya Waombolezaji walijitokeza kuuaga mwili wa Marehemu 
Sajini wa Magereza Peter Shelukindo aliyekufa kwa ajali ya gari Wilayani
 Mkuranga(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa 
Magereza, Dkt. Juma Malewa.
إرسال تعليق