![]() |
| Ay, Salama na Josh wakiwa Kenya |
Mkasi ni kipindi cha TV kilichoanzishwa na msanii na
mfanyabiashara Ambwene Yessaya aka AY, kipindi kilichojipatia umaarufu
mkubwa nchini Tanzania.
AY yuko nchini Kenya ambako pamoja na mambo mengine ameenda kuzindua video yake mpya ya ‘Asante’ iliyotoka weekend iliyopita.
Kwa mujibu wa Nairobi Wire, AY ameenda Kenya na crew ya Mkasi ambao
ni Salama Jabir na Josh Murunga, kwa ajili ya kuangalia fursa zinazoweza
kupatikana nchini humo kwa lengo la kutaka kupanua wigo wa kipindi
hicho.
“Tuko hapa kwanza kuangalia uwezekano wa kupanua biashara ya kipindi chetu” Alisema AY.
Wiki iliyopita msimu wa mkasi ulimalizika kwa Salama kumhoJi AY, na
moja ya vitu alivyovisema AY kuhusu kipindi ni pamoja na hiki:
“Season inayokuja itakuwa ni revolution kama ambavyo tumefanya
mwanzo…kwa kweli ni kuwa watu ambao wana akili zao watu ambao wana lengo
moja kwa pamoja ni timu ambayo inafanya kitu pamoja na tunafanya kitu
kimoja ambacho kinawafundisha na watu wengine”.
Msimu mpya wa Mkasi ambayo hurushwa kupitia EATV unatarajiwa kuanza Julai Mosi.

Post a Comment