
Meneja
uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, akizungumza na
waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza zawadi za
washindi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambapo Azam FC ambaye
ndie bingwa atanyakua Milioni 75. Pamoja nae katika picha, wa kwanza
kutoka kulia niAfisa Habari wa TFF, Boniface Wambura na Afisa Matukio
na Udhamini wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude.

Meneja
uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, (Katikati)
akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza
zawadi za washindi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambapo Azam FC
ambaye ndie bingwa atanyakua Milioni 75. Timu za Yanga, Mbeya City na
Simba zilizomaliza nafasi ya pili hadi ya nne zitavuna 37M, 26M na 21M
zote zikiwa na nyongeza ikilinganishwa na kiasi walichozawadiwa timu
zilizoshika nafasi hizo msimu uliopita wa 2012/2013.Pamoja nae katika
picha, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga, (Kushoto)
Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura (Kulia)

Meneja
Uhusiano wa Nje Vodacom Tanzania, Salum Mwalimu akizungumza na waandishi
wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza zawadi za washindi wa
ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambapo Azam FC ambaye ndie bingwa
atanyakua Milioni 75. Timu za Yanga, Mbeya City na Simba zilizomaliza
nafasi ya pili hadi ya nne zitavuna 37M, 26M na 21M zote zikiwa na
nyongeza ikilinganishwa na kiasi walichozawadiwa timu zilizoshika nafasi
hizo msimu uliopita wa 2012/2013.Wa kwanza kutoka kushoto katika picha
ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga, Afisa Habari
wa TFF, Boniface Wambura na Afisa Udhamini na Matukio wa Vodacom,
Ibrahim Kaude.

Meneja
Uhusiano wa Nje Vodacom Tanzania, Salum Mwalimu akisisitiza jambo kwa
waandishi wa habari, wakati wa kutangaza zawadi za washindi wa ligi kuu
ya Vodacom Tanzania Bara, ambapo Azam FC ambaye ndie bingwa atanyakua
Milioni 75.Timu za Yanga, Mbeya City na Simba zilizomaliza nafasi ya
pili hadi ya nne zitavuna 37M, 26M na 21M zote zikiwa na nyongeza
ikilinganishwa na kiasi walichozawadiwa timu zilizoshika nafasi hizo
msimu uliopita wa 2012/2013.Pamoja nae katika picha, wa kwanza kutoka
kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga, Afisa
Habari wa TFF, Boniface Wambura na Afisa Udhamini na Matukio wa
Vodacom, Ibrahim Kaude.
![]() |
| Baadhi ya Waandishi wa habari walioudhuria katika mkutano wa kutangaza zawadi kwa timu za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.Ambapo Azam FC ambaye ndie bingwa atanyakua Milioni 75. Timu za Yanga, Mbeya City na Simba zilizomaliza nafasi ya pili hadi ya nne zitavuna 37M, 26M na 21M zote zikiwa na nyongeza ikilinganishwa na kiasi walichozawadiwa timu zilizoshika nafasi hizo msimu uliopita wa 2012/2013. |
* Timu yenye nidhamu kuvuna 16M
Mdhamini
Mkuu wa Ligi kuu Vodacom Tanzania Bara kampuni ya Mawasiliano ya
Vodacom imetangaza kuipatia timu ya Azam FC kitita cha Sh 75 kama zawadi
ya fedha taslimu baada ya kuibuka bingwa wa ligi msimu wa 2013/2014.
Mwaka jana Bingwa wa Ligi Kuu Vodacom ambapo ilikuwa timu ya Yanga alizawadiwa kitita cha Sh 70 Milioni.
Zawadi
hiyo imetangazwa leo jijini Dar es salaam na Meneja Uhusiano wa Nje wa
Vodacom Salum Mwalim katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika
Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania - TFF.
"Tunayofuraha
kubwa leo kuzitangaza zawadi za fedha taslimu kwa bingwa wetu mpya na
wengine walioshika nafasi ya pili hadi ya nne, tunajisikia furaha
kutimiza yale yaliyo kwenye mkataba wetu wa udhamini wa ligi."Alisema
Mwalim
Timu za
Yanga, Mbeya City na Simba zilizomaliza nafasi ya pili hadi ya nne
zitavuna 37M, 26M na 21M zote zikiwa na nyongeza ikilinganishwa na kiasi
walichozawadiwa timu zilizoshika nafasi hizo msimu uliopita wa
2012/2013.
Mwalim
amesema Vodacom itaendelea kufanya kila lililo ndani ya uwezo wake
kuboresha ligi ikiwemo zawadi ili kuongeza kasi ya ushindani miongoni
mwa timu shiriki za ligi.
Amesema
Vodacom itatumia zaidi ya Sh 210 kwa ajili ya zawadi za fedha kwa timu
zilizoshika nafasi nne za juu pamoja na timu nyengine zilizoonesha
umahiri katika maeno mengine ikiwemo timu yenye nidhamu itakayovuna 16M.
"Tunatambua
kuwa bado zipo changamoto za hapa na pale ikiwemo eneo la zawadi, na
matazamio na matarajio ya watanzania hususan wapenda soka bado ni
makubwa lakini angalau sasa tumefika mahala tunapoweza kujivunia hadhi
na mahala ligi ilipo wakati safari ya mafanikio zaidi ikiendelea."
Wengine
watakaovuna fedha kutoka Vodacom ni pamoja mchezaji bora (5.2M),
mfungaji bora (5.2M), mlinda mlango bora 5.2M), mwamuzi bora na mwalimu
bora 7.8 kila mmoja.
"Shabaha
yetu ni kutafuta namna bora ya ligi yetu kuwa bora zaidi ya hapa
tulipofika ili kuvutia wawekezaji zaidi, ni kwa njia hiyo tutafikia
mafanikio makubwa zaidi ya kuwa na ligi kubwa, yenye ushindani na mvuto
wa juu zaidi ndani na nje ya nchi..'Alisema Mwalim
Mwalim
ametumia nafasi hiyo kuendelea kuzipongeza timu zote 14 zilizoshiriki
ligi huku akiutaja msimu wa 2013/2014 kuwa ulikuwa bora zaidi ya msimu
uliopita wa 2012/2013.
Mwisho.

إرسال تعليق