Baba aliyetajwa kwa jina moja la Nuhu maarufu kama ‘Mzee Kijana’ (54) anusurika kifo baada ya fumanizi Aprili 19 (Ijumaa Kuu), mwaka huu maeneo ya Tuangoma Mjimwema, Kigamboni jijini Dar. |
KIFO njenje!
Baba aliyetajwa kwa jina moja la Nuhu maarufu kama ‘Mzee Kijana’ (54),
nusu auawe na raia wenye hasira kali, msimu wa Pasaka kisa kikiwa ni
kuachiwa kwa dhamana isiyoeleweka baada ya kunaswa kwa kosa la ulawiti
wa madenti.
Tukio hilo la kutisha lilijiri Aprili 19 (Ijumaa Kuu), mwaka huu maeneo ya Tuangoma-Mjimwema,…
KIFO njenje!
Baba aliyetajwa kwa jina moja la Nuhu maarufu kama ‘Mzee Kijana’ (54),
nusu auawe na raia wenye hasira kali, msimu wa Pasaka kisa kikiwa ni
kuachiwa kwa dhamana isiyoeleweka baada ya kunaswa kwa kosa la ulawiti
wa madenti.
Baba
aliyetajwa kwa jina moja la Nuhu maarufu kama ‘Mzee Kijana’ (54)
anusurika kifo baada ya fumanizi Aprili 19 (Ijumaa Kuu), mwaka huu
maeneo ya Tuangoma Mjimwema, Kigamboni jijini Dar.
Tukio hilo la kutisha lilijiri Aprili 19 (Ijumaa Kuu), mwaka huu maeneo
ya Tuangoma-Mjimwema, Kigamboni jijini Dar, mbele ya ofisi ya serikali
ya mtaa huo ambapo awali, Aprili 9, mwaka huu ilidaiwa kuwa mzee huyo
alidakwa na mmoja wa wazazi wa wanafunzi hao akiwa amemfungia kwa kufuli
mwanaye ndani ya chumba chake huku mwenyewe akiwa katika shughuli zake
za kuuza kuni.
Picha inaonyesha gari lililotumika kumchua mpaka kituoni.
Ilisemekana kwamba akiwa na mjumbe wa kitongoji hicho, mzazi huyo
aliyepata fununu kuwa mwanaye wa kiume analawitiwa na mzee huyo,
alifanya jitihada za kumsaka mzee huyo hadi kibaruani kwake ambapo
alipohojiwa kama amemfungia mwanafunzi wake ndani ya chumba chake, mzee
huyo alijiumauma na mwishoni kukubali.
Mzee huyo akijaribu kujificha kwa aibu.
Ilidaiwa kwamba wananchi na mzazi wa mwanafunzi huyo walimbeba mzee huyo
msobemsobe hadi nyumbani kwake na kumtaka amfungue denti huyo ambapo
alifanya kama alivyoagizwa kisha mwanafunzi huyo alichomolewa ndani ya
chumba hicho.
Habari
zilieleza kuwa sakata hilo lilitinga katika ofisi ya mtendaji ambapo
walitoa taarifa kwa askari wa Kituo cha Polisi cha Kizuiani. Hata hivyo,
ilisemekana kwamba askari hao walishindwa kufika kwa kuwa siku hiyo
daraja la Kongowe lilikuwa limeharibika.
Ilisemekana
kuwa baadaye walipata msaada kutoka kwa polisi wa Kituo cha Kibada,
Kigamboni ambao walimchukua mtuhumiwa na baadaye kupelekwa Kizuiani kwa
ajili ya taratibu za kisheria huku mwanafunzi huyo akipewa PF-3 kwa
ajili ya uchunguzi kama kweli alikuwa akiingiliwa kinyume na maumbile.
Baadhi ya raia wenye hasira kali wakiwa nje ya kituo cha polisi alipofikishwa mtuhumiwa huyo.
Ilidaiwa kuwa kabla hata majibu ya daktari hayajachukuliwa, Mzee Kijana
alionekana akirandaranda mitaani, jambo lililosababisha viongozi wa mtaa
huo kuwasiliana na polisi kuhoji kulikoni?
Ilielezwa kuwa wakati wakuu hao wakihangaika na suala hilo ndipo wananchi wenye hasira kutoka kila upande waliivamia ofisi hiyo wakidai kuwa wamechoshwa na rushwa za wazi zinazofanywa na viongozi wao na kudai kuwa watampa adhabu mzee huyo wao wenyewe.
Ilielezwa kuwa wakati wakuu hao wakihangaika na suala hilo ndipo wananchi wenye hasira kutoka kila upande waliivamia ofisi hiyo wakidai kuwa wamechoshwa na rushwa za wazi zinazofanywa na viongozi wao na kudai kuwa watampa adhabu mzee huyo wao wenyewe.
Ilidaiwa kwamba kufumba na kufumbua, watu hao wasio na idadi walivunja
mlango na kumchomoa Mzee Kijana aliyekimbilia ofisini humo kwa ajili ya
hifadhi na kuanza kumshambulia kwa kila aina ya silaha kiasi cha
almanusura kumuua.
Kipigo hicho kilisababisha askari waliofika hapo ili kutuliza ghasia,
kushindwa kazi, jambo lililowalazimu kutoka nduki ili kuokoa roho zao.
Akizungumza na wanahabari wetu, mwenyekiti wa mtaa huo, Mohamed Chande
alisema kuwa ilibidi aikimbie ofisi yake kwa kuwa watu walikuwa na
ghadhabu kupita maelezo.
Inadaiwa kuwa msamaria mwema mmoja alimnyakua Mzee Kijana kutoka katika
kundi la watu na kumpakiza kwenye gari lake haraka na kumsalimisha
mikononi mwa Polisi wa Kizuiani ambapo inadaiwa kuwa hadi sasa yupo
huko.
Akizungumza na waandishi wetu, bibi wa mwanafunzi huyo anayedaiwa
kulawitiwa aliyejitambulisha kwa jina moja la Rugwesi (38), alisema kuwa
alishangaa kuona mtuhumiwa akiachiwa kwa dhamana siku chache kabla hata
majibu ya daktari hayajatoka.
“Ripoti imeonesha kuwa mjukuu wangu alikuwa akilawitiwa kwa muda mrefu
na mzee huyo na si mjukuu wangu tu inadaiwa anawafanyia hivyo wanafunzi
wengine watatu,” alisema bibi huyo huku simu ya mkuu wa Kituo cha Polisi
Kizuiani ikiita bila kupokelewa.
Post a Comment