Baadhi
ya Wanachama wa Chama cha Wanafunzi wa Udaktari Tanzania { TAMSA } kwa
kushirikiana na wizara ya afya Zanzibar wakiendesha zoezi la siku nne
la kupima, kutoa elimu na huduma za Dawa kwa wagonjwa wa maradhi ya
Kisukari na Shinikizo la Damu hapa Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipima damu mara
baada ya kufungua kampeni ya kutoa huduma za shinikizo la Damu na
Kisukari katika majengo ya Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni
MnaziMmoja Mjini Zanzibar.
Mradi
huo unasimamiwa na Jumuiya ya Chama cha Wanafunzi wa Udaktari Tanzania {
TAMSA } kwa kushirikiana na Chuo mcha Kimataifa cha Udaktari Tanzania {
imtu }.
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar balozi Seif akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Kimataifa cha
Udaktari Tanzania { IMTU } Profesa Flora Fabian Mbatia kwenye majengo ya
Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ .
Na Othman Khamis Ame, oMPR
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba ukosefu wa mlo kamili
uliokusanya matunda na mboga za kutosha, uvutaji wa sigara na unywaji wa
pombe kiholela, tabia ya uvivu na ongezeko la uzito ndio sababu kuu
zinapelekea ongezeko kubwa la maradhi ya Kisukari na shindikizo la Damu
miongoni mwa wanaadamu.
Alisema utumiaji wa
vyakula hivyo kwa mpango maalum pamoja na ushauri unaotolewa na
wataalamu wa afya ndio njia pekee inayoweza kuzuia kuripuka kwa maradhi
hayo kwa zaidi ya asilimia 80%.
Balozi Seif alisema
hayo katika sherehe ya ufunguzi wa Kampeni ya kutoa huduma za Shindikizo
la Damu na Kisukari zilizoandaliwa na Jumuiya ya Chuo cha Udaktari
Tanzania na kufanyika ndani ya Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha
Zanzibar Kampasi ya Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni Vuga Mjini
Zanzibar.
Balozi Seif Ali Iddi
alilazimika kuzifungua sherehe hizo ndani ya Ukumbi kufuatia amri ya
Jeshi la Polisi Tanzania kuzuia mikusanyiko ya aina yoyote kwenye maeneo
mbali mbali Nchini katika kipindi hichi.
Awali sherehe hizo
zilipangwa kufanyika katika uwanja wa michezo wa Maisara Suleiman Mjini
Zanzibar ambapo Jeshi la Polisi likaamuru zivunjwe kwa kuondosha
mkusanyiko wa watu.
Balozi Seif alisema
maradhi ya Kisukari na Shindikizo la Damu ambayo yamekuwa tishio la vifo
vingi hapa Nchini yamesababisha matatizo mengi ya Kiuchumi na Kijamii
kiasi cha kuzibebesha mzigo familia, Taifa na Dunia kutokana na gharama
za matibabu yake.
Alieleza kwamba
Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni { WHO } za mwaka 2012 zinaonyesha
zaidi ya watu Milioni 4.8 wamepoteza maisha kutokana na maradhi hayo
wakati ambapo Dola za Kimarekani zaidi ya Bilioni 471 zimetumika katika
kupambana na janga hilo.
Alifahamisha kwamba
utafiti uliofanywa kwa upande wa Zanzibar imeonyesha kuwa asilimia 33%
ya Wananchi wa Zanzibar wanasumbuliwa na tatizo la shinikizo la Damu na
asilimia 3.7% wamepatwa na maradhi ya Kisukari.
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar alieleza kwamba inakadiriwa ifikapo mwaka 2030 zaidi ya
Dola za Kimarekani Bilioni 500 zinatarajiwa kutumika katika kupambana na
na maradhi ya Kisukari na Shinikizo la Damu ulimwenguni kote.
Alitanabaisha kwamba
hicho ni kiasi kikubwa cha fedha ambacho jamii ikiweza kujiepusha na
vishawishi vya maradhi hayo Mtaifa yanaweza kuokoa kiasi hicho ambacho
kinaweza kutumiwa katika Nyanja mbali mbali za maendeleo.
Balozi Seif alieleza
kuwa huo ni mtihani mkubwa ambao Binaadamu wanahitajika kuwa makini kwa
kila aina ya ushauri unaotolewa na wataalamu tofauti wa sekta za afya na
kuhakikisha kwamba unafuatwa vilivyo.
Aliupongeza Uongozi na
wanachama wote wa Chama cha Wanafunzi wa Udaktari Tanzania { TAMSA }
pamoja na Chuo Cha Udaktari Tanzania { IMTU } kwa moyo wao wa kujali
ustawi wa Wananchi Bara na Zanzibar na kuahidi kwamba Serikali
itajitahidi kuunga mkono juhudi zao hizo.
Alisema Chama cha
Wanafunzi wa Udaktari kimekuwa kikifanya kazi kubwa katika kuzisaidia
Serikali zote mbili kwenye sekta muhimu ya afya. Hivyo Serikali haina
budi kuiunga mkono katika kusaidia changamoto zinazoikabili Taasisi hiyo
hususan suala zima la kupatikana kwa Jengo kwa ajili ya Ofisi yao.
Balozi Seif aliuomba
Uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar { SUZA } katika Kitivo cha
Utabibu kufanya mazungumzo na Taasisi hiyo ya Tamsa ili kuangalia
utaratibu wa kujiunga kwa lengo la kutoa nafasi ya pekee ya Vijana wa
Zanzibar nao kuihudumia Jamii inayowazunguuka.
Katika kuunga mkono
jitihada za Wanachama hao wa Chama cha Wanafunzi wa Udaktari Tanzania {
TAMSA } za kupima kutoa huduma na dawa bure za Maradhi ya Kisukari na
Shinikizo la Damu ndani ya siku Nne hapa Zanzibar Balozi Seif aliahidi
kutoa mchango wa shilingi Milioni 1,000,000/- kusaidia Chama hicho.
Mapema Mapema
Mwenyekiti wa Chama cha Wanafunzi wa Udaktari Tanzania { TAMSA }
ambae pia ni msimamizi Mkuu wa Mradi wa Kampeni ya kutoa huduma za
shinikizo la Damu na Kisukari Nd. Siraji Mohammed Mtulia alisema
chimbuko la mradi huo linatokana na ongezeko kubwa la maradhi hayo
katika jamii Nchini.
Siraj Mohammed alisema
mradi huo unakududiwa kutoa huduma za afya, elimu pamoja na Dawa kwa
wagonjwa wanaosumbuliwa na Maradhi ya Shinikizo la Damu na Kisukari
katika mikoa yote Mitano wa Zanzibar.
Alisema licha ya mradi
huo kupata ufadhili wa Taasisi za Kitaifa na Kimataifa zinazojihusisha
na masuala ya Afya lakini utaendelea kuwa wa kudumu kwa kusaidia jamii
kutoa elimu ya afya kwa njia ya kujitolea.
Akitoa salamu katika
sherehe hizo Mkuu wa Chuo cha Kimataifa cha Udaktari Tanzania { IMTU }
Profesa Flora Fabia Mbatia alisema mradi huo ni wa kwanza kufanyika
Nchini Tanzania ukilenga kuongeza ufahamu wa Taaluma ya kujikinga na
maradhi yasiyoambukiza.
Profesa Flora
alibainisha kwamba mradi huo uko sambamba na dhana ya Serikali zote
mbili katika kushajiisha jamii kupitia sekta ya afya kupiga vita maradhi
mbali mbali yanayowasumbuwa Wananchi.
Naye kwa upande wa
Wizara ya Afya Zanzibar Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dr. Saleh Mohammed
Jidawi aliitanabahisha jamii kushirikiana na Serikali katika kupiga
vita maradhi hayo ya Kisukari na Shinikizo la Damu kutokana na hatai
yake kushinda haya yale maradhi ya kuambukiza.
Dr. Jidawi alieleza
kwamba maradhi hayo yanaua, yanaleta ulemavu, gharama za tiba yake iko
juu sana kiasi kwamba jamii inapaswa kubadilisha tabia kwa matumizi ya
vyakula visivyo na tija.
Post a Comment