
MWANAISHA – “Chidi naona uko na mama watoto”
CHIDI BENZ – “kusogea karibu nikakuta ni Mwanaisha na wenzake, ndio
nikamwambia mbona unanichora au kwasababu nipo na dem mkali kuliko
wewe?…..unaona wivu?…. kilichofata ni chupa ambayo Mwanaisha aliirusha
ikanipata kichwani na kunipasua damu zikatoka ndipo mimi nikamshika
nywele Mwanaisha na baada ya hapo kilichofata sikumbuki maana nilikua nimelewa” (Kwa Mujibu wa DJFetty blog)
nywele Mwanaisha na baada ya hapo kilichofata sikumbuki maana nilikua nimelewa” (Kwa Mujibu wa DJFetty blog)
Hii ni sababu ambayo Chidi Benz msanii mkubwa tu hapa nchini ameitoa
kupitia “Gossip Cop Soody Brown” wa segment cha “You Heard” ndani ya XXL
ya Clouds FM baada ya mtangazaji huyo kwenda kumtembelea kituo cha
polisi cha sehemu hiyo mitaa ya ILALA magorofani.
Kweli kwa msanii ambae anaongoza kwa mskendo za kupiga watu ambao
hawajawahi kusema, watangazaji wa maradio, wasanii wenzake na
kuwasababishia majeraha makubwa kwa kipindi kirefu anaweza akatoa sababu
kama hiyo ambayo imefikia kumsababishia maumivu makali mwanadada
“Mwanaisha” ambae hata kama kweli alimuita na kumwambia maneno hayo yeye
kama kioo cha jamii alitakiwa kufanya matendo hayo kweli?…. Chidi Benz
ni msanii mzuri sana mwenye kipaji lakini hivi sasa mashabiki wake
wameacha kusikiliza muziki wake na kukaa kusikiliza skendo ambazo ni
uchafu wa tabia isiyokubalika katika jamii ya karne hii, huwezi kuamka
na kuanza kumshambulia binadamu mwenzako haswa mwanamke na kuweza
kumsababishia majeraha ya kuweza kushonwa nyuzi 18.
Haya ni matendo ambayo Jamii haitakiwi kukubaliana nayo kwa watu kama
hawa, vyombo vya habari visibaki kukimbizana na kuwasaidia kupromote
nyimbo zao na kuwachekea na umaarufu wao wakati huku kwenye jamii
wanafanya mambo yasiyostahili kuwepo kwa watu wa aina hiyo sababu
wanaishia mtaani kuhatarisha usalama wa wananchi haswa haswa wanawake
ambao ndio wanaoonewa sana na watu hawa. Juzi tumetoka kusikia DUDU BAYA
amemkata sikio “Mama yake amkubwa” ambae ni mwanamke mwenye umri mkubwa
kutokuwa na nguvu za kuhimili na kuzuia shambulio la mtu “Mwanaume”
mwenye mwili mkubwa kama DUDU BAYA huko Mwanza na leo tunakuja kusikia
Chidi Benz amefanya kitendo hicho hicho kwa mwanamke hapa Dar Es Salaam.
Hata kama ni wasanii na wanajulikana na kujuana na Police, lakini
haki lazima itendeke tena kwa mfano dhahili kama wao ni vioo vya jamii
ili wananchi wa kawaida wasije wakafwata matendo hayo yasiyo mazuri.
Matendo hayo tumeona hata nchini Marekani msanii “Chris Brown” baada ya
kumshambulia “Rihanna” pamoja na umaarufu wake wote, hivi sasa
anatumikia kifungo Jela baada ya kutoka Rihab kwa makosa yake
aliyoyatenda.
Chidi Benz ambae kutokana na vyombo vya habari kuwa anashikiliwa na
polisi baada ya kesi kwenda mahakamani ambapo Mheshimiwa “Hakimu”
ameamuru kuendelea kushikiliwa kwa kwa msanii huyo baada ya hali ya
Mwanaisha kuwa mbaya kiasi cha kushindwa kuongea.

Post a Comment