Dunia ina mambo! Baba amvutisha mtoto wake wa miaka miwili sigara!

Dunia inazidi kuharibiwa na viumbe wanaoishi ndani yake hasa binadamu! Video ya kushtua inayomuonyesha baba mwenye asili ya Russia akimruhusu kwa kumpa mtoto wake mdogo anayekadiriwa kuwa na miaka miwili kuvuta sigara huku akifurahia kabisa kitendo hicho imevuja!!



Huku wakiendelea kuvuta sigara hiyo yaani baba na mwana huyo anayetia huruma kutokana na umri wake mdogo kimesikika kicheko cha mwanamke kwa nyuma sasa sijaelewa ni mama wa mtoto alikuwa akifurahia kinachofanyika au vipi!

Ikafika kipindi baba akawa anaendelea kuvuta bila kumpasia dogo basi mtoto akaangua kilio akinyooshea pakti ya sigara fresh iliyokuwepo mezani na bila hiyana bazazi huyu akavuta sigara moja na kumuwashia..poor kid!

Post a Comment

Previous Post Next Post