Alisema amekuwa mtu asiyetetereka hata pale alipokuwa akitoa kauli ambazo hazikuwapendeza baadhi ya watu.
Akizungumza jana katika hafla iliyofanyika
katika viwanja vya ofisi ya CCM Wilaya ya Mwanga, Rais Kikwete alisema
Msuya amekuwa kiongozi wa kuigwa na Watanzania pamoja na viongozi walio
madarakani, kwa kutopenda kuendelea na madaraka kama ilivyo kwa
wengine.
"Wanamwanga
mmefanya jambo la heri la kumuaga mzee wenu angali akiwa hai, tofauti
na watu wengi huagwa wakiwa wameshatwaliwa dunia huku akimwagiwa sifa
nyingi ambazo hawezi kusikiaÉhili ni jambo jema kutambua mchango wake
katika taifa angali akiwa hai,Ó" alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete
alisema serikali itazidi kutimiza wajibu wake wa kuendelea kumhudumia,
kumuenzi na kuthamini mchango wake katika nyanja mbalimbali za
maendeleo, ikiwa ni pamoja na kuchangia kukuza uchumi wa nchi katika
kipindi chake alichotumikia taifa.
Pia Rais alimuomba Mzee Msuya
kutumia muda wake wa mapumziko kuandika historia ya maisha yake katika
utumishi wa umma na vipande vya historia ya nchi, ili aweze kuacha
hazina muhimu kwa taifa na uzoefu wake uweze kutumika.
Awali
akitangaza kustaafu kwake Mzee Cleopa Msuya Mwenye umri wa miaka 83,
alisema ameamua kustaafu shughuli zote za siasa ambazo amezitumikia kwa
kipindi cha miaka 33, na atabaki kuwa mwanachama mwaminifu na mkereketwa
wa CCM.
Msuya anastaafu kazi zote za siasa akiwa ametumikia taifa
tangu mwaka 1955 hadi mwaka 2012 akiwa ameshika nyadhifa mbalimbali za
uwaziri katika wizara tofauti, uwaziri mkuu, makamu wa kwanza wa rais
pamoja na nyadhifa nyingine za juu za CCM.
Post a Comment