Mkuchika
alitaja Serikali za Mitaa kuongoza kwa kuwa na malalamiko 65 ikifuatiwa
na Idara ya Mahakama iliyokuwa na malalamiko 46 huku Idara za Polisi na
sekta binafsi zikiwa na malalamiko 35 kila moja.

Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Utawala Bora, George Mkuchika aliyasema hayo jana mjini hapa
alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Kikao cha Ushauri cha Mkoa wa Mbeya
(RCC) kwa lengo la kutoa elimu ya utawala bora kwa wajumbe hao.
Alisema kutoka
halmashauri kulikuwa na malalamiko 18,Tanesco kulikuwa na malalamiko
matatu huku Idara za Uhamiaji, Maliasili, Serikali Kuu, vyombo vya
habari, taasisi za dini na Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) zilikuwa na lalamiko moja kila moja.
Waziri huyo alisema bado
kuna ushirikiano mdogo wa wadau katika kukabili rushwa. Alitaka jamii
ibadilike na kutoa ushirikiano wa kutosha badala ya kuachia wizara na
Takukuru pekee.
Wajumbe wa kikao hicho waliomba kubadilishwa kwa
sheria ya Takukuru ili iweze kuipa meno taasisi hiyo kwa kuruhusu
kuchunguza na kushitaki yenyewe pasipo kupeleka mashitaka kwa Mkurugenzi
wa Mashitaka (DPP) hatua waliyosema imekuwa ikichelewesha uendeshaji wa
mashitaka.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Chrispin Meela aliitaja wilaya
yake kuwa miongoni mwa maeneo nchini ambayo kuna mashitaka mengi ya
Takukuru ambayo hayakuweza kuendeshwa kutokana na Ofisi ya Mkurugenzi wa
Mashitaka kuchelewa kurejesha majibu.
Post a Comment