Rapper D-Knob amesema baaada ya kuachia single yake ‘Nishike
Mkono’ aliyomshirikisha Mwasiti iliyotoka mwezi wa pili, anatarajia
kuachia single mbili mpya kwa pamoja mwezi ujao (May).
Akizungumza na Bongo 5, D-Knob ambaye jina lake halisi ni Innocent
Sahani amesema ameamua kutoa single mbili kwa wakati mmoja lakini moja
itakuwa kwenye video tu na ya pili itatoka audio.
“Wiki hii hapa au wiki ijayo nashoot video ingine” amesema D-knob,
“ambayo nategemea itoke mapema sana ikiwezekana tarehe moja mwezi wa
tano au mwisho wa mwezi huu, watu ntawaeleza zaidi nyimbo inahusu nini
na nini lakini hii nyimbo ntaitoa kwenye video tu…kwa sasabu kwenye
audio kuna nyimbo nyingine nataka nitoe kwenye radio, na-surprise kama
nyimbo mbili kwa wakati mmoja, moja itakuwa kwenye audio moja itakuwa
kwenye video, inaweza kupishana siku moja lakini ni wakati mmoja.”
D-Knob amesema video anayotarajia kutoa atafanya na director Nick
Dizzo ambaye pia alihusika kutengeneza video ya ‘Nishike Mkono’.
“Video mpaka sasa hivi nipo karibu na Nick Dizzo ambaye alifanya
nyimbo ya Nishike Mkono, kwasababu naamini jamaa anajua level gani
ameniacha kwenye Nishike Mkono…”.
Ameongeza kuwa ana mpango wa kwenda Cape Town, Afrika Kusini kufanya video ya moja ya nyimbo hizo atakazoziachia hivi karibuni.
“Jana tulikuwa tunachora script, idea ya kwanza hii video nilitaka
kwenda kushoot Cape Town, nikamwambia Nick tukashoot Capetown,
tukakubaliana fresh, lakini jana kanipigia simu akaniambia skiliza, hii
hata tukishoot Capetown, kutokana na script ambayo tumeichora lazima pia
tuishoot na bongo. Kwa hiyo conclusion ambayo tumeipata jana mi na Nick
ni kwamba hii video tuitengeneze kwanza bongo.” Alisema Mr Sahani.
Pamoja na mpango huo kubadilika lakini amesisitiza kuwa bado
ataendelea na mpango wa kwenda kufanyia video Cape Town kwa wimbo
mwingine.
“Inaweza isiwe nyimbo hii lakini lazima kwa sababu nilikuwa
nishaandaa hiyo, kwahiyo hiyo plan sitaifuta nitaiacha kama ilivyo,
kwahiyo nyimbo itakayotoka kwenye audio ikija kuhamia kwenye video
lazima ntaenda kushoot kule. Sio kwa sababu nikishoot kule lazima nyimbo
itakuwa kali sana yaani mimi mwenyewe nahisi kufanya hivyo…mimi
mwenyewe napenda kwenda na changes ambazo zinafanyika katika maisha,
halafu ukichukulia Cape Town ni sehemu ambayo ndugu zangu wako pale
wanaishi, kwahiyo mimi nahisi nahitaji kwenda kubadilisha mazingira.”
D-Knob amesema kuwa ‘Nishike mkono’ imemrudisha vizuri katika game
sababu toka imetoka mwezi wa pili imeshampa show kubwa zisizopungua
tano.
Msikilize zaidi
إرسال تعليق