
Kila
mechi itakayochezwa leo itatoa heshima ya mwisho kwa kocha wa zamani wa
Barcelona, Tito Vilanova kwa wachezaji na mashabiki wote kusimama kimya
kwa dakika moja.
Shirikisho la Soka la Hispania limeagiza timu zote kusimama na kufanya hivyo, leo, kesho na keshokutwa.
Mechi ya
kwanza ambayo itashiriki katika kutoa heshima kwa Vilanova aliyefariki
jana akiwa na umri wa miaka 45 ni ile itakayozikutanisha Elche dhidi ya
Levante.
Lakini
hata shirikisho la mpira wa kikapu nchini humo limeagiza mechi zote za
wikiendi kuwe na kipande hicho cha dakika moja kutoa heshima kwa
Vilanova na mechi ya kwanza kufanya hivyo itakuwa ile kati ya ya Real
Madrid dhidi ya Olympiacos ambayo ni ya michuano ya kikapu barani Ulaya.
إرسال تعليق