Katika kipindi cha ALA
za ROHO cha CLOUDS FM, Mtangazaji/Msanii Diva The Boss akiwa na Rapper
WAKAZI alisema kuwa, NIKKI MBISHI ni msanii mzuri sana na anafanya
vizuri ila yeye binafsi anachoona ni kwanini
anakosa kuwa na heshima kwa wasanii wenzake na watu wengine sio jambo
zuri na aanze kuwa na RESPECT, na hii ni kutokana na matendo anayodai ya
sio kuwa na heshima ya kuandika na kudiss wasanii wenzake kwenye
mitandao ya kijamii. WAKAZI nae alisema yeye hana beef na msanii yoyote
na anashangaa madai ye yeye kuwa na ‘Beef’ na msanii Nikki Mbishi na
Godzillah. Vile vile alisema kuwa wasanii wengi wanaotaja majina ya watu
kwenye nyimbo zao mara nyingi hutakaga attention kwa kutumia majina ya
watu kwenye nyimbo zao ili wasikike, wakazi hakutaka kuiongelea sana
hiyo issue na wasanii hao wakatoka kwenye hiyo topic.
WAKAZI msanii ambae ameanza muziki wake muda mrefu kidogo akiwa kule
nchini Marekani na ametoka kuachia nyimbo zake mbili kwa mpigo, “Sexy
Lady” na “Sumu ya Panya”, alisema Tanzania hatuna uzalendo wa kusifia na
kusupport cha kwao. hii ni kutokana na swali aliloulizwa na Diva kuwa,
kwanini nini tunasupport sana nyimbo za Nigeria na zinapigwa sana kwenye
Clubs za hapa nchini kuliko nyimbo za wasanii wa hapa nyumbani.
Wasanii hawa walizungumzia jinsi gani nchi kama Uganda inavyosupport
wasanii wao kwa kazi zao na hata show zao na kuwafanya wasanii hao
kuweza kuwa na maisha mazuri na kuweza kuendelea kutengeneza muziki
mzuri wenye hadhi ya kimataifa.
إرسال تعليق