
Dogo Janja ameiambia Bongo5 kuwa kwa sasa anaweza kufanya kitu
chochote hata akiwa mwenyewe kwa kuwa muziki umemlea na amekua nao.
“Mkataba wangu umeisha safi na Ostaz Juma,kila mtu yupo kiroho safi
na mwenzake,mimi kwa sasa nipo solo artist lakini najua naenda wapi kwa
sasa. Mimi hapa ni msanii ambaye nimeshakuwa na mimi kama mimi naweza
nikasema muziki umenilea. Mimi nimekulia kwenye huu muziki naelewa
changamoto zake na matatizo yake,kwanza nakuwa nausoma huu muziki na
naulewa huu muziki unavyokwenda. Sasa nipo solo artist na ninaweza
kujiunga na kundi lolote,team yangu ya taifa ni watoto wa bibi ,nipo
tayari kujiunga na kundi lolote lakini itakuwa kwa mikataba maalum,”
amesema.
Dogo Janja amesema yapo makundi ya Arusha yanayomsaidia mpaka atakaposimama vizuri.
“Mtaani kwetu kuna kitu kinaitwa ‘Watoto Wa Bibi’ haw watoto wa bibi
kuna Jambo Squad, kuna Maker Cheka,kuna Dogo Janja na wengine mengi haya
ni makundi tofauti lakini vipo katika sehemu moja. Tunasaidiana kwa
namna moja hama nyingine mpaka pale mtu ambapo anakuwa amesimama
vizurI.”
Post a Comment