Elton John kufunga ndoa na mpenzi wake mwezi wa tano mwaka huu.

b5efd0dad9e5e0b886da8cbc9b3e5f7b0213f7da
Pop Star Elton John amefunguka na kusema kua siku si nyingi atafunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi David Furnish. Ameyasema hayo mara baada ya Uingereza kuruhusu ndoa za jinsia moja, David Furnish ni raia wa Uingereza. Hapo awali Elton alishindwa kufunga ndoa na mpenzi wake huyo kutokana na ndoa za Jinsia moja kupigwa marufuku nchini Uingereza.
Akihojiwa na kituo cha NBC’s  Elton alisema ” Tutafanya ndoa yetu kimya kimya” Wapenzi hao ambao wamejaariwa kupata watoto wawili pamoja katika uhusiano wao wanatarajiwa kufunga ndoa yao mwezi wa 5 huko England. Ndoa ambayo itakua ni ya kiserikali na mashahidi wataohudhuria ni watoto wao wawili pamoja na mashahidi wachache. Hiyo ni kwa mujibu wa maneno ya ELton

Post a Comment

أحدث أقدم