Ukiambiwa utaje nyimbo za Rama Dee zilizofanya vizuri, huwezi
kuacha kuutaja wimbo wake ‘Kikao cha Family’ ama kinavyojulikana pia kwa
jina la ‘Usijali Mpenzi’. Hapa Rama Dee anasimulia utunzi wa wimbo huo.
Yaa hiyo ngoma nilifanya na jamaa wa Iringa ipo na story nzuri
sana. Tulienda kwenye show Iringa mimi na Joh halafu jamaa anaitwa Amba
alikuja hotel akiwa na nyimbo zangu zote za nyuma, akaniambia anaomba
afanye kazi na mimi halafu kwa jinsi alivyo kuja kirahisi tukajua si
mkali kwenye kupiga midundo, mbaya zaidi kwake mbali kutokea sehemu
tulipofikia kipindi kile.
Joh alikuwa wa kwanza kutoamini kama jamaa mzuri kwenye midundo
(beats) ila nikaona ngoja niende nimpe Moyo jamaa. Nilipo fika kwake cha
kwanza nilishangazwa na jinsi studio yake ilivyo na mpangilio na
nidhamu ya hali ya juu kwa mwanamuziki. Jamaa baada ya kuwasha computer
na kufungua kazi zake nilisikia kama nipo kwenye sehemu yenye upepo
mzuri maana alinishangaza sana. Watu wa mikoani wanaweza sana naamini na
jamaa aliweza kupata nafasi ya kusikika Tanzania nzima nipo na amani na
furaha kubwa kwa sasa maana nilifanya kitu ambacho alikiona kabla
yangu, ametisha sana wimbo ni mkubwa sana. Mpaka leo nikisikiliza “Kikao
Cha family” huwa namuona Amba kabisa.
Pia baada ya hapo nilijifunza kufanya kazi na Ma-producer wanaochipukia ni msaada mkubwa sana kwa pande zote mbili haswa kwa msanii cha kwanza unapata ladha tofauti isiosikika mara kwa mara, pili unapata kuwafundisha na kuwapa ujasiri kwenye ubunifu wa kupiga kazi au “Midundo, Tatu kuwaepusha Na- propaganda za kitanzania…mpaka sasa kwa nyimbo zangu zote nilifanya na watu ambao walikua hawajasikia sana na sasa wapo sehemu nzuri akiwepo Makochali alitengeneza “Sina Time” pale Kama kawa. Jors Bless Dj wa Times FM alitengeneza “Sio waoaji” na nyingine nyingi..
Pancho, Nahreel mpaka kufikia Ally da bway ambae ni dogo kabisa ameweza kutengeneza wimbo mkubwa kama “Kama Huwezi”. Napenda sana wasanii wote Tanzania iwe Mchongaji au mchoraji nk…pia napenda kusaidia sehemu ambazo naweza kusaidia, katika wasanii ambao nimetumia nguvu kubwa kuwasaidia nafikiri ni Mapacha Maujanja saplayaz wao nimewapigia chorus zaidi ya 10 kuanzia kipindi cha Pasu kwa pasu mpaka leo ila sikuchoka mpaka nilihakikisha nawaacha sehemu ambayo wataweza kuendelea, nasikia wanaendelea vizuri mimi sijui sijawasiliana nao muda sana toka wajisalimishe (teh teh teh).
Usikilize wimbo huo (Kikao cha Family) hapa

Mtu ambae najivunia mpaka sasa ni Nikki wa pili. Yeye ni
msanii ambaYe siwezi kumuelekeza sana ila alinishangaza muda mrefu
uandishi wake. Sikutumia nguvu sana kwa maana alikua na uwezo wa kipekee
kwenye “Good Boy” mpaka kufikia hapa leo. So ni sehemu ndogo au kubwa
ambazo naweza kusema zinanipa furaha. Ni vigumu kusimama kimaisha kama
unacheza mchezo wa kinafiki, mimi sipendi wanafiki.
Post a Comment