Miaka michache ijayo M-Pesa, Tigo Pesa au Airtel Money zinaweza kuwa na mpinzani mwingine, Facebook Pesa!!
Katika miaka ijayo Facebook haitakuwa sehemu tu ya kuandika status,
kupost picha ama kusoma kinachoendelea mjini bali itakuwa sehemu ambapo
watumiaji wataweza kufanya malipo ya kieletroniki na kutunza fedha pia.
Mtandao huo wa kijamii unadaiwa kuwa kwenye mchakato wa kuingia kwenye
utoaji wa huduma za kifedha ambapo pamoja na mambo mengine, wafanyakazi
waliopo nchi za kigeni wanaweza kutuma fedha kwa familia zao.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka The Financial Times, Facebook imetuma
maombi kwenye benki kuu Ireland, ambapo kama ikipewa itawaruhusu watu
kutunza fedha kwenye mtandao huo wa kijamii, kuhamisha kwa watumiaji
wengine na kulipia bidhaa ama bili.
Pia mtandao huo umezungumza na makampuni mapya ya huduma hizo ya
London, TransferWise, Moni Technologies na Azimo ambayo yanatoa huduma
za utumaji fedha kwa njia ya apps za smartphone
إرسال تعليق