
Unapoingia katika penzi jipya, ni kipindi ambacho moyo wako unakuwa
na furaha ya hali ya juu. Unaweza kuhisi unaibeba dunia nzima kwa raha
ya penzi jipya, utajitahidi kumuonesha huyo uliyempata kila aina ya
mahaba ilimradi aendelee kuwa na wewe na akupende zaidi.
Lakini kadiri unavyozidi kukaa na mwenzako na mnavyozidi kuzoeana, ndipo unapopata nafasi ya kuyajua maisha yake kwa undani.
Taratibu utaanza kufahamu yeye ni mtu wa aina gani, kabla yako
alikuwa na nani (ex wake), anatokea kwenye familia ya namna gani au
anaishi katika mazingira gani.
Hapo ndipo matatizo yanapoanzia. Yawezekana kuna mambo mengi
alikuficha wakati mnakutana lakini sasa unaanza kuyabaini wewe mwenyewe.
Hiki ni kipindi kigumu ambacho wengi hushindwa kukivuka na matokeo
yake, kukaa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa wiki kadhaa au miezi kadhaa
ndiyo inaonekana fasheni.
Utafiti
mwepesi unaonesha kuwa wanawake au wanaume wengi wanaingia kwenye
uhusiano mpya baada ya ule wa awali kuvunjika au kulegalega. Ni wachache
sana wanaoingia katika uhusiano ambao mwenzi wako hajawahi kuwa na
mpenzi au amekaa kipindi kirefu bila kutoka na mtu yeyote.
Kwa mantiki hiyo, unapoingia katika penzi jipya, unatambua kwamba
wewe siyo wa kwanza. Kuna wenzako walishatangulia kabla yako ambao
mwenzi wako ndiye anayewajua kwa majina na sura.
Pia utafiti mwingine unaonesha kwamba hakuna jambo gumu kama kutengana katika uhusiano wa kimapenzi.
Pia utafiti mwingine unaonesha kwamba hakuna jambo gumu kama kutengana katika uhusiano wa kimapenzi.
Kwamba hata kama mwenzako ameshakwambia hakutaki, itakuchukua muda
mrefu sana kuamini kwamba kweli anamaanisha kile alichokisema.
Katika kipindi cha mwishomwisho wakati uhusiano wa kimepenzi
ukielekea mwisho, lazima yule anayeachwa atakuwa anaendelea kubembeleza
apewe nafasi nyingine au asamehewe kama kuna jambo alikosea.
Kwa bahati mbaya, wengi wetu huwa hatujipi muda wa kutosha unapotoka
kwenye penzi la awali kuingia kwenye penzi jipya. Matokeo yake, wengi
wanajikuta wameanzisha uhusiano na mtu mwingine katika muda ambao mpenzi
wa awali bado hajaliafiki suala la kutengana.
Bado anabembeleza na kuamini anaweza kupata nafasi nyingine ya kurekebisha pale alipokosea ili maisha ya kimapenzi yaendelee.
Kinachotokea sasa, unakuta umekaa na mpenzi wako mpya lakini bado
yule wa zamani anakupigia simu au anakufuatilia mitaani akitaka kupata
muda wa kuzungumza na wewe ili myamalize na kuendelea na uhusiano.
Ni hapo ndipo unapopata nafasi ya kujua kuwa kumbe mpenzi wako
alikuwa anatoka na mtu mwingine na bado anampenda ndiyo maana anampigia
simu ukiwa naye, anamfuata kila anakokwenda na wakati mwingine anakuja
hata ukiwa na mpenzi wako mpya.
NINI CHA KUFANYA KUKABILIANA NA HALI HIYO?
Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna mtu anayeweza kufurahia kugundua mpenzi wake bado ana mawasiliano na mtu wake wa zamani. Ni katika kipindi hiki, wengine uzalendo unawashinda na kuamua kukubali kukaa pembeni kuepusha msongamano.
NINI CHA KUFANYA KUKABILIANA NA HALI HIYO?
Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna mtu anayeweza kufurahia kugundua mpenzi wake bado ana mawasiliano na mtu wake wa zamani. Ni katika kipindi hiki, wengine uzalendo unawashinda na kuamua kukubali kukaa pembeni kuepusha msongamano.
Hata hivyo, hutakiwi kuwa mwoga, kupandwa na jazba, kupigana, kutukanana au kuvunjiana heshima na x wa mpenzi wako
إرسال تعليق