Gazeti la Vatican laiponda filamu ya ‘Noah’, laiita ni filamu ya ‘Nuhu pasipo Mungu’.

noah-poster-russell-crowe-teaser

Muigizaji wa filamu ya hadithi ya biblia, Noah, Russell Crowe alihangaika mwezi March kutafuta mkutano ambao ungeonekena kama kuungwa mkono (endorsement) kwa filamu hiyo na Papa Francis na Vatican. Kwa mujibu wa gazeti la jana la Vatican liitwalo Avvenire, staa huyo hakuweza kufanikiwa.
Gazeti hilo la Avvenire limeiita filamu ya Noah “fursa iliyopotea’, na Nuhu bila Mungu. Liliendelea kuwa kuandika kuwa filamu imeuelezea mkasa wa Nuhu na gharika kama nafasi iliyopotezwa. Crowe, muongozaji wa filamu hiyo, Darren Aronofsky na mtayarishaji, Scott Franklin pamoja na mwenyekiti wa kampuni ya Paramount, Rob Moore wote walisafari kwenda Vatican, March 19.
Kwa ufupi timu hiyo ilikutana na kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani aliyewabariki pamoja na watu wengine 40,000 kwenye kanisa la St. Peter’s Square lakini filamu hiyo haikujadiliwa.
Filamu hiyo imepigwa marufuku kuoneshwa kwenye nchini nyingi za Kiislamui duniani.

Post a Comment

أحدث أقدم