
Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited – Dodoma
Hii
ni baada ya washindi watatu kutoka Kanda ya Kati kupatikana katika
shindano la kusaka vipaji vya kuigiza lililoendeshwa na Kampuni ya Proin
Promotion Limited (PPL). Fainali ya kuvisaka vipaji kwa kanda ya Kati
ilifanyika jana Mnamo tarehe 15 April 2014 Mkoani Dodoma na washindi
kutangazwa na Jaji Mkuu wa shindano hilo, Roy Sarungi aliyesaidiwa na
Yvonne Chery ‘Monalisa’ na Single Mtambalike ‘Richie Richie.’Roy
kwa kusaidiana na Yvonne Chery ‘Monalisa’ na Single Mtambalike ‘Richie
Richie.’ aliwatangaza Joyce Rebeca, Moses Obunde na Mwinshehe Mohamed
kuwa washindi wa shindano la kusaka vipaji vya kuigiza Tanzania
lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents ambapo kila mmoja alipewa
zawadi nono ya Sh 500,000. Shindano hilo liliwashirikisha washiriki 500,
lakini ni washiriki watano wenye vipaji waliofanikiwa kuingia tano bora
na baadaye majaji walifanya kazi kubwa ya kuwachagua na kuwatangaza
washindi watatu.
Mshiriki mkubwa kuliko wote
, Idrisa Ally (40), alionesha kipaji cha hali ya juu cha kuigiza na
alizawadiwa na majaji Sh 100,000. Idrisa hatakwenda kushiriki fainali za
mashindano hayo zinazotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu jijini Dar es
Salaam kutokana na umri wake kuwa mkubwa kuliko kigezo cha umri
kilichowekwa cha kuanzia miaka 14 hadi 35, ingawa majaji waliahidi
kuwasiliana naye kwa lengo la kuendeleza kipaji chake umri wake
utakaporuhusu.
“Tumebaini kuwa Kanda ya
Kati hususani Mkoa wa Dodoma kuna vipaji vingi vya sanaa ya uigizaji na
katika hili Idrisa Ally ametuthibitishia yeye ni mzee mwenye kipaji,
lakini amedhihirisha kuwa ana kipaji cha kuigiza,” anasema Jaji Mkuu wa
shindano hilo, Sarungi anasema sanaa ya uigizaji ni muhimu kwa vijana,
kwa vile sasa hutoa fursa ya ajira ambapo imewawezesha vijana wengi
nchini kujiajiri wenyewe na kuimarika kiuchumi.
“Ni matumaini yangu kuwa
kwa washindi hawa wa Kanda ya kati hawataishia hapa watajiendeleza zaidi
kwani uigizaji sasa ni ajira,” anasema. Mshiriki Moses Obunde
alishindwa kuzuia furaha yake baada ya kutangazwa mshindi, aliangua
kilio kuashiria furaha aliyokuwa nayo na kuufanya ukumbi mzima
kutaharuki.
Ofisa Uhusiano wa Proin
Promotion Limited (PPL), Josephat Lukaza, ambao ndio waratibu na
waandaaji wa shindano hilo la kusaka vipaji vya uigizaji, anasema
mashindano hayo yanaendeshwa kikanda, ambapo kwa kuanzia walianza kusaka
vipaji kwa Kanda ya Ziwa na Kumalizika Jana katika Kanda ya kati Mkoa
wa Dodoma na hatimaye zoezi hili kuamia Kanda ya Juu Kusini ambapo
usaili utafanyika Mkoani Mbeya kuanzia tarehe 19 April.
“Baadaye tutaelekea Kanda
ya Njanda za Juu Kusini lakini tunashukuru kwa ushirikiano tulioupata
kwa wakazi wa Kanda ya Kati, tumepata washiriki 600, ambao tuliwachuja
hadi kuwapata washindi watatu waliokidhi vigezo tulivyovihitaji,”
anasema Lukaza. Baadhi ya vigezo kwa mujibu wa Lukaza, vilikuwa ni
mshiriki kuwa na umri kuanzia miaka 14 hadi 35, anayejiamini, mbunifu,
anayemiliki jukwaa na igizo lake libebe ujumbe wa kuelimisha.
Anasema lengo la PPL
kuzungukia kanda hizo sita nchini ni kuhakikisha kuwa inavisaka vipaji
vya vijana kupitia sanaa ya maigizo, ambavyo vimejificha ili viendelezwe
na kampuni yake. “Tumeamua kuwekeza katika sanaa maana sanaa ni fursa
kama zilivyo fursa zingine nchini na ni matumaini yetu kuwa jamii
itatuunga mkono katika safari ndefu tuliyo nayo ya kuvisaka na
kuviendeleza vipaji,” anaeleza ofisa huyo uhusiano.
Anasema PPL inaendesha shindano hilo kwa kanda sita nchini ambazo ni Kanda ya Ziwa, Magharibi, Pwani, Kati, Kaskazini na Kusini.
“Kwa sasa tumeanza na mikoa
sita, lakini matarajio yetu ya baadaye ni kuifikia mikoa yote nchini
ambapo tunaamini kuna vipaji vingi vya wasanii vimejificha ili waweze
kupata ajira kupitia vipaji vyao,” anasema na kuongeza kuwa mshindi wa
jumla baada ya mashindano ya kikanda kumalizika atapatikana Agosti mwaka
huu jijini Dar es Salaam, ambako ataondoka na zawadi nono ya Sh milioni
50.
Anasema usakaji vipaji
hivyo huendeshwa kwa umakini na umahiri mkubwa kupitia kwa majaji na
watu wenye utalaamu wa tasnia ya filamu na teknolojia ya habari (IT)
walio chini ya kampuni yake, ambao pia huzingatia miiko na maadili ya
kazi hiyo kwa kila mshiriki. Anasema PPL imesajiliwa rasmi mwaka 2013
kupitia Sheria ya Usajili wa Makampuni ambayo hushughulika na ukuzaji wa
sanaa ya filamu nchini.
“Pia tunashughulika na
usimamizi wa uzalishaji wa filamu nchini, uzalishaji na usambazaji wa
DVD na filamu zilizokamilika kuingia sokoni na matarajio yetu ya baadaye
ni kuwa kampuni bora katika Bara la Afrika,” anaeleza. Wakizungumza na
gazeti hili, washindi waliobuka kidedea waliwashukuru waandaaji wa
shindano hilo kwa kuibua vipaji vyao ambavyo wanasema visingeweza
kutambulika.
Crecensiah anasema
anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumwibua katika shindano hilo na
kumwezesha kuwa mshindi, ambapo sasa anaamini kuwa ndoto yake ya kuwa
msanii wa kimataifa imetimia. “Namshukuru Mungu kwa yote, lakini zaidi
niwashukuru waandaaji wa shindano hili kwa kutumia muda wao na fedha
kuvisaka vipaji, binafsi naona kiu yangu ya kuwa muigizaji wa kimataifa
imetimia, nitaongeza juhudi kubwa katika tasnia ya filamu,” anasema
msanii huyo. Naye Janeth anasema penye nia pana njia, kwa madai kuwa
alikuwa na kiu ya kuwa msanii wa kuigiza kwa muda mrefu hasa baada ya
kuwaona wasanii mbalimbali kupitia luninga nchini.
“Kwa kweli naweza kusema
nimepata maji ya kunywa dhidi ya kiu yangu ya kuwa msanii, ni kazi
ambayo nilikuwa naipenda tangu nikiwa mtoto namshukuru sana Mungu na
waandaaji wa shindano hili la kusaka vipaji vya kuigiza,” anaeleza
mshindi huyo. Kwa upande wake, Joshua Wambura anasema ushindi wake ni
mwanzo wa safari yake ndefu katika kuingia katika tasnia ya filamu ndani
na nje ya nchi.
إرسال تعليق