Mbu anayeambukiza kidinga popo
Nchini Tanzania watu 147 wamethibitika kuwambukizwa ugonjwa wa homa
ya kidinga popo yaani homa ya dengu huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki
dunia kwa ugonjwa huo.
Kasi ya ugonjwa huo ambao ikiwa hautadhibitiwa unaweza kuleta madhara
dalili zake zinashabihiana na zile za malaria kwani unaambukizwa kwa
kupitia mbu na unadaiwa kusambaa katika maeneo mengine nchini Tanzania
ingawa kwa sasa uko zaidi mjini Dare salaam.
Taarifa zinasema kuwa kuna visa vya wagonjwa nchi jirani ya Msumbiji
taifa linalopakana na mkoa wa Mtwara jambo linalozua wasiwasi wa kuwa na
visa vingine mkoani humo. Kutaka kufahamu hatua zinazochukuliwa na
serikali ya Tanzania Joseph Msami amezungumza na Dk Janet Mgamba ni
kaimu mkurugenzi msaidizi wa udhibiti na ufuatailiaji wa magonjwa ya
milipuko ambaye anaanza kwa kueleza hali ya kidinga popo ilivyo.
(SAUTI MAHOJIANO)

إرسال تعليق