Kwa Rihanna hua sio ‘big deal’ kupost picha za utupu katika
mitandao ya kijamii, inavyoonekana ni moja ya starehe zake ambazo
zimeonekana kuvuka mipaka iliyowekwa na wamiliki wa mtandao wa kushare
picha wa Instagram.
Mwimbaji huyo wa Barbados, jana aliweka picha za utupu katika mtandao
wa Instagram, lakini wamiliki wa mtandao huo waliziondoa picha hizo
kwasababu zilikiuka masharti yanayozuia watumiaji kutoweka picha za aina
hiyo katika mtandao huo.
Chanzo kiliuambia mtandao wa TMZ kuwa Instagram licha ya kuziondoa
picha hizo pia walimtumia barua pepe ya kumuonya vinginevyo watamfungia
kutoutumia mtandao huo.
Hata hivyo Riri bado aliendelea kupost picha hizo katika mtandao wa Twitter.
إرسال تعليق