Jina ‘Nyong’o’ lawazingua ‘Reporters’ Duniani, Kulitamka - VIDEO

url
Ni siku chache zilizopita Lupita Nyong’o  alitangazwa kuwa mwanamke mzuri sana  kwa mwaka 2014 na jarida la “People Magazine”. Lupita alipata umaarufu sana baada ya kuigiza vizuri katika filamu ya ’12 Years A Slave’.
Moja ya kitu kigumu zaidi kumhusu Lupita ni namna ya kutaja jina lake la pili ‘Nyong’o’, ikiwa ni siku chache tu baada ya Lupita kupewa hesima hiyo na People Magazine youtube kuliwekwa video inayoonyesha jinsi waandishi wa habari wanavyoshindwa kulitaja kwa ufasaha jina hilo. Video hiyo iliyowekwa tarehe 26 ya mwezi huu imepata zaidi ya watazamaji 216,000 hadi wakati tunaandika habari hii.
Unaweza itazama video hiyo hapa chini

Post a Comment

Previous Post Next Post