
Jokate
Mwegelo yupo single ... Staa huyo mwenye vipaji lukuki alisema hayo
Jumatatu hii kwenye kipindi kipya cha TV1, ‘The One Show’
anachokiendesha kwa kushirikiana na Ezden Jumanne aka The Rocker.
Katika kipindi
hicho cha kwanza kuoneshwa, watangazaji hao walianza kwa kuhojiana wao
kwa wao kwanza na moja ya maswali aliyoulizwa Jokate ni kama yupo kwenye
uhusiano wowote wa mapenzi. Jokate ambaye pamoja na kuwa muigizaji wa
filamu pia ni muimbaji wa muziki na mjasiriamali, alisema kuwa kwa sasa
yupo single lakini haimaanishi kuwa wanaume hawamsumbui kumtaka
kimapenzi.
Jokate amewahi
kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mchezaji wa basketball wa timu ya
Oklahoma City Thunder, Mtanzania Hasheem Thabeet pamoja na uhusiano
uliodumu kwa kipindi kifupi na staa wa muziki, Diamond Platnumz.
إرسال تعليق