
Justin Bieber ni mmoja
wa wasanii wachache kabisa wanaofatiliwa sana na vyombo vya habari
dubiani kwa sasa, Siku za karibun Justin amenaswa na vyombo mbalimbali
vya habari akifanya matendo ambayo yamewaacha watu midomo wazi. Machache
kati ya hayo ni kukamatwa na madawa na ya kulevya, kelewa kupitiliza na
kuendesha gari kwa kasi huku akijua kabisa leseni yake imeisha mda wa
matumizi. Matendo haya yalifikia kufikishwa Ikulu ya nchini Mareaki
“White House” na baadhi ya wananchi wa nchi hiyo kutaka afutiwe ‘Hati’
yake ya kuishi nchini humo ili arudi kwao nchini Canada.
Justin ambaye kwa sasa yupo nchini Japan huku akiwa kasindikizwa na
mama yake mzazi ‘Patti Mallette’ na watu wa karibu wa Justin Bieber.
Akiwa nchini humo Justin aliamua kutembelea kituo cha kulelea watoto
yatima kilichopo nchini humo, Kupitia akaunti yake ya Instagram Justin
aliweka video ikimwonyesha akicheza na watoto hao.
Tukio la Justin Bieber kutembelea kituo hicho limechukuliwa tofauti
huku wengine wakimpongeza kwa kutembelea kituo hicho huku wengine
wakisema kua Justin kaamua kufanya hivyo ili kuwalaghai watu ili wasahau
mabaya yake.
إرسال تعليق