![]() |
| Picha hiyo inamuonesha Justin Bieber akiwa mbele ya kanisa hilo na kuandika: “Thank you for your blessings.” |
Justin Bieber amekinukisha tena. Safari hii si kwa kujua na ni
baada ya kuwaudhi Wachina na Wakorea Kusini kwa kupost picha kwenye
Instagram ya kanisa lenye utata la nchini Japan.
Staa huyo wa Canada aliweka picha ya kanisa hilo la Yasukuni la
jijini Tokyo ambalo ni kumbukumbu ya watu milioni 2.5 waliouwa miongoni
mwao wakiwa wahalifu wa kivita. Kanisa hilo ni tata kwa nchi za China na
Korea Kusini ambalo wanaliona kama kitu cha Japan kujivua udhalimu na
ukatili ulioufanya pale ilipoyashika maeneo mengi ya China na Korea
wakati wa vita vita vya pili vya dunia.

Baada ya watu wengi kumshambulia kwenye Instagram, Bieber aliifuta
picha hiyo na kuandika post nyingine ya kuomba radhi kwa kuandika: “While
in Japan I asked my driver to pull over for which I saw a beautiful
shrine. I was mislead to think the shrines were only a place of prayer.
To anyone I have offended I am extremely sorry. I love you China and I
love you Japan.”

إرسال تعليق