Mwanamitindo Kim Kardashian anaendelea kujipanga zaidi kwa
ajili ya siku ya ndoa yake na rapper Kanye West ambayo inatarajiwa kuwa
moja kati ya matukio yatakayoteka vichwa vingi vya habari May 24 mwaka
huu.
Chanzo kimoja kimeliambia jarida la Grazia kuwa Kim Kardashian
ameanza kulala na kivazi maalum ‘corset’ ambacho kinasaidia kutengeneza
umbo lake ili awe na muonekano mzuri zaidi katika siku hiyo ya ndoa.
“Kim wants her figure to look absolutely perfect on her wedding day.
Wearing a corset at night is extremely uncomfortable but has a proven
record of results, and with six weeks to go, Kim is up for anything.”
Kimesema Chanzo hicho.
Imeelezwa kuwa Kim amejipanga kutengeneza muonekane wake ikiwa ni
pamoja ngozi wakati wanafamilia hao watakapokuwa mapumzikoni nchini
Thailand.
إرسال تعليق