Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Kigoma mjini bila kujali
mvua,ambapo alisisitiza kuwa CCM itatekeleza kila walichoahidi.
Kila mtu alijikinga na mvua kwenye uwanja wa Mwanga Community Centre
Viti vikitumika kujikinga na mvua
iliyokuwa inanyesha wakati wa mkutano wa CCM uliofanyika kwenye viwanja
vya Mwanga Community Centre wilaya ya Kigoma mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (wa kwanza
kulia),Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma Dk. Aman Walid Kaborou, Balozi
Karume na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya wakiwa
wamesimama kwenye jukwaa kuu wakati wa mkutano wa hadhara bila kujali
mvua kubwa iliyokuwa inanyesha.
Mbunge wa Kigoma mjini Mheshimiwa
Peter Serukamba akiwahutubia wakazi wa Kigoma mjini kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre na
kuwaambia kuwa Kigoma imebadilika na bado anapigania wananchi hao wapate
maji salama na ya kutosha.
Upinde wa Mvua unaonekanika kabla mvua
kubwa haijanyesha kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre ambapo
mkutano mkubwa wa CCM ulikuwa unafanyika.
:
Mjumbe wa NEC Balozi Ali Abeid Karume
akiwahutubia wakazi wa Kigoma mjini na kuwaambia kuwa Muungano wa
Serikali mbili ndio Muungano pekee utakaodumisha Umoja miongoni mwa
wananchi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye akihutubia umati wa wakazi wa Kigoma mjini kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre ambapo
aliwaambia kuwa vyama vya upinzani vinaelekea kutoweka mapema kabla hata
havijakomaa kidemokrasia.
Asisitiza Umoja na Mshikamano Kigoma
Asema ahadi zote zitatekelezwa
Awataka Viongozi wa CCM kufanya mikutano mingi na wanachama na wananchi kwa jumla
Nape afundisha Umma Demokrasia ya
kweli,aonyesha namna gani vyama vingi vya upinzani ni wababaishaji
atolea mifano namba alivyotelekezwa mgombea wa Chalinze
Zaidi ya wanachama 350 wajiunga na CCM
إرسال تعليق