![]() |
| Ndugu wa marehemu Elitha Kaizilege wakipeleka mwili wa ndugu yao kanisani kwa ajili ya maombi. |
HIKI ni kioja! Ndugu wa marehemu Elitha Kaizilege ambaye alipatwa na mauti katika Hospitali ya Kairuki iliyopo Mikocheni jijini Dar wiki iliyopita, walifanya tukio la aina yake baada kutokukubali kama ndugu yao amefariki.
Kana kwamba haitoshi, baada ya muda huo kupita, ndugu hao, wanaosadikika kuwa ni waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima, waliupeleka kanisani hapo ambapo uliombewa zaidi ya saa mbili mwili huo ili uamke, ikashindikana.
Mchungaji Gwajima akiwa kazini.Wakati akiumwa, inadaiwa kuwa tatizo kubwa lililokuwa likimsumbua ni sikio lakini katika vipimo kadhaa alivyopimwa, havikuonyesha ugonjwa.
Kwa mara ya mwisho kuna madai kuwa alikuwa na kansa ya kichwa, kitu ambacho pia kiliwashangaza ndugu ambao walishangaa ni wapi alipoutoa ugonjwa huo mara moja.
Inadaiwa pia kuwa wakati akiumwa, mama huyo aliwahi kupigiwa simu na mtu anayehisiwa ni mganga wa kienyeji kutoka Kigoma, ambaye haikufahamika walichoongea.
Inasemekana kuwa mara tu baada ya madaktari wa Hospitali ya Kairuki kuwataarifu kuhusu kifo cha mgonjwa wao, walizuia mwili huo kupelekwa chumba cha maiti wakiamini hajafariki, na kwamba wanataka wafanye maombi ili kumfufua.
Baada ya maombi ya hospitalini na kanisani kushindikana, mchungaji aliyeongoza ibada hiyo,
ambaye jina lake halikuweza kujulikana mara moja, aliwaambia ndugu hao
kuwa marehemu hataweza kuamka na kuwataka waupeleke mwili huo chumba cha
kuhifadhia maiti. Waandishi wetu walimtafuta kiongozi mkuu wa kanisa hilo mchungaji Josephat Gwajima ili aweze kuzungumzia suala hilo, lakini waliambiwa kuwa yuko Japan kwa kazi ya kuhubiri neno.Hata hivyo, mmoja wa viongozi waandamizi wa kanisa hilo, aliyekataa jina lake kutajwa gazetini, alisema maombi ya aina hiyo hufanyika kanisani hapo na mara kadhaa, watu waliodhaniwa wamefariki waliweza kuinuka.

إرسال تعليق