KLINIKI YA AIRTEL RISING STARS YAFIKIA TAMATI.

Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Levi Nyakundi akiongea na waandishi wa habari wakati wa kufunga kliniki ya kimataifa ya soka ya siku tano ya Airtel Rising Stars kwenye uwanja wa Azam Compex. Kliniki hiyo ilileta pamoja vijana zaidi ya 70 kutoka nchi 12 Barani Afrika.
Kocha Neil Scott kutoka shule za soka ya vijana za Manchester United akiongea kwenye sherehe za kufunga kliniki ya soka ya kimataifa ya Airtel Rising Stars kwenye uwanja wa Azam Compex. Kliniki hiyo ilileta pamoja vijana zaidi ya 70 kutoka nchi 12 Barani Afrika. Pamoja naye ni Andrew Stoke kutoka MUSS and Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Levi Nyakundi.
.Washiriki watajuwa kuwa na malengo ya kujiunga na timu zao za taifa pamoja na klabu zinazoshiriki ligi kuu. 
.Mwisho wa kliniki ni mwanzo wa msimu wa wa Airtel Rising Stars kwa nchi 17. 
Kliniki ya siku tano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars imefikia tamati jana huku washiriki wakiwa na shauku kubwa ya kutumia ujuzi waliopata kwa kuwa nyota wa soka kwenye nchi zao na hata wa kimataifa. 
Kliniki hio iliodhuriwa na washiriki zaidi ya 70 kutoka nchi za Kenya, Malawi, Sierra Leone, Burkina Fasso, Chad, Congo Brazzaville, DRC, Niger, Madagascar, Gabon, Shelisheli na wenyeji Tanzania. Makocha kutoka shule za soka ya vijana wa Manchester United ndio walioendesha kliniki hiyo. 
Kliniki hiyo imetoa fursa kwa washiriki kuendelea kukuza vipaji vyao chini ya programu ya shule za soka ya vijana za Manchester United, ambazo ni maarufu kwa kufundisha jinsi ya kucheza kandanda safi na la kushambulia. Makocha hao wawili – Neil Scott na Andrew Stokes walikuwa wakitoa mafunzo kwa kuengemea upande wa ufundi, ujuzi na nidhamu ndani na nje ya uwanja. 
‘Makocha kutoka Manchester United kwa kushirikiana na Airtel wamefanya kazi kubwa kuwafundisha hawa vijana na naomba shirikisho la Mpira katika kila nchi pamoja na vilabu vya ligi kuu kuwapa nafasi kuendeleza vipaji vyao,’ alisema Levi Nyakundi, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania wakati wa kufunga kliniki hiyo kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi. 
Aliongeza, ‘Airtel inatambua baadhi ya vijana wa Airtel Rising Stars wamekuwa wakishiriki kwenye timu za vijana tangu kuanzishwa kwa programu hii. Ni matarajio yetu kwamba washiriki wengi wa Airtel Rising Stars watapata nafasi ya kucheza kwenye timu za miaka chini 20. Tumepata nguvu ya kuendelea kuwekeza kwenye programu hii kwa sababu tumeweza kuona mafanikio yake.’ 
Airtel Rising Stars ni mpango kambambe kwa Afrika kuwapa fursa kwa wasichana na wavulana wenye umri chini ya miaka 17 kuonyesha vipaji vyao kwa waalimu waliobobea kwenye masuala ya kandanda na kupata nafasi ya kuziendeleza. 
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake Rogasiana Kaijage ambaye amefuatilia mafunzo hayo tangu mwanzo hadi mwisho amesisitiza umuhimu wa klabu kuwekeza kwenye vijana wenye umri wa chini kulikon kutumia fedha nyingi kununua wachezaji ambao umri ushakwenda. Kaijage amesema programu kama hizi zinasaidia kupata vipaji chipukizi lakani kazi ya kuviendeleza inabakia kuwa ya klabu. 
Kumalizika kwa kliniki nii kutoa nafasi nyingine kwa Airtel Rising Stars kuzindua awamu ya nne ya programu hii ambayo uanzia kwenye ngazi ya kata mpaka Taifa kwa nchi kumi 17 Barani Afrika, ambapo Airtel inafanya biashara.
Mchezaji wa timu ya Sierra Leone ya Airtel Rising Stars Fatmata Mansaroly, akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Levi Nyakundi baada ya kumalizika kwa kliniki ya soka ya kimataifa ya Airtel Rising Stars kwenye uwanja wa Azam Compex. Kliniki hiyo ilileta pamoja vijana zaidi ya 70 kutoka nchi 12 Barani Afrika. Kushoto ni Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando
Mchezaji wa timu ya Tanzania ya Airtel Rising Stars Joseph Prosper, akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Levi Nyakundi baada ya kumalizika kwa kliniki ya soka ya kimataifa ya Airtel Rising Stars kwenye uwanja wa Azam Compex. Kliniki hiyo ilileta pamoja vijana zaidi ya 70 kutoka nchi 12 Barani Afrika. Kushoto ni Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando.
Timu ya Tanzania ya Airtel Rising Stars wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kliniki ya siku tano ya soka ya kimataifa ya Airtel Rising Stars kwenye uwanja wa Azam Complex. Waliokaa kutoka kushoto ni – Kocha mkuu wa timu ya Wanawake Tanzania Rogasian Kaijage, Mkurugenzi Masoko Airtel Tanzania Levi Nyakundi na Makocha kutoka shule za soka ya vijana za Manchesterb United Neil Scott na Andrew Stokes.

Post a Comment

Previous Post Next Post