Kocha Yanga atangaza anaowatema .


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm.
SIKU chache baada ya kumalizika kwa msimu wa 2013/2014, hatimaye Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm amekamilisha ripoti yake na kuiwasilisha kwa uongozi wa timu hiyo.
Haruna Niyonzima.
Pluijm ambaye alichukua jukumu la kuinoa timu hiyo wakati wa katikati ya msimu uliopita, ameonyesha kuwa mkali na ambaye anahitaji kufanya vizuri zaidi msimu ujao baada ya kushika nafasi ya pili katika msimu huu.
Ripoti hiyo ya kocha huyo ambayo Championi Jumamosi imepata dondoo zake ni kuwa amepanga kuwa na sura mpya kadhaa na pia wale ambao wataonekana hawana faida kwake na hawamo kwenye mipango yake, ameruhusu waondoke na hayo yatatendeka ikiwa uongozi wa klabu yake utayafanyia kazi.
Athuman Idd ‘Chuji’
Baadhi ya wachezaji waliomo kwenye kikosi hicho ambao ameruhusu waondoke kwa sababu mbalimbali ni Haruna Niyonzima, Athumani Idd ‘Chuji’, Jerry Tegete, Shaban Kondo, Rajab Zahir, Ibrahim Job, Salum Telela na Ally Mustapha ‘Barthez’.
Mtoa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo amelithibitishia gazeti hili kuwa, hao ni baadhi yao ambao wametajwa kwenye ripoti hiyo.
Mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi.
“Niyonzima anaondolewa kwa kuwa kocha hamhitaji kwenye mipango yake, Chuji sababu kubwa ni utovu wa nidhamu, hao wengine ni suala la viwango,” alisema mtoa taarifa.
Kitu cha ajabu kilichoibuka kwenye ripoti hiyo ni kuwa kocha huyo amesema anamhitaji mshambuliaji Reliants Lusajo ambaye mara nyingi amekuwa ‘bize’ na shule kiasi cha kushindwa kuonekana mara kwa mara kwenye timu.
Jerry Tegete.
“Amesema anamtaka Lusajo, sababu kubwa ni kuwa ana kiwango kizuri licha ya kuwa hajacheza mechi nyingi lakini pia ana elimu nzuri, anajua anaweza kuwa kioo kwa wachezaji wengine,” alisema mtoa taarifa huyo.
Pluijm, raia wa Uholanzi, ambaye juzi alikuwa Uwanja wa Taifa, akifuatilia mchezo wa kujipima nguvu baina ya timu ya taifa ya vijana (U-20) dhidi ya Taifa Stars, alizungumza na gazeti hili na kuweka wazi mambo kadhaa.
 
Kipa wa Yanga, Ally Mustapha ‘Barthez’.
“Kuhusu ripoti yangu, hilo ni suala langu na utawala wa klabu, labda cha kukwambia ni kwamba watu watarajie kuona sura mpya nyingi msimu ujao na kuna sura hazitakuwemo, lakini hayo yatafanyika iwapo ripoti niliyowasilisha itafanyiwa kazi vilivyo,” alisema Mholanzi huyo.
Aidha katika ripoti hiyo haijamzungumzia mshambuliaji Mganda Emmanuel Okwi, ambaye aliweka mgomo wa kutocheza mechi za mwisho za ligi kuu kwa madai kuwa hajamaliziwa fedha zake za usajili, japokuwa kiongozi huyo alishatanza kuwa Okwi, hayumo kwenye mipango yake msimu ujao.

Post a Comment

أحدث أقدم