
Ripota
wa TZA nchini Kenya Julius Kipkoitch anaripoti kwamba ni watu wanne
wameuawa baada ya gari lilokua likielekeea katika kituo cha polisi cha
Pangani kilometa mbili kutoka Eastleigh jijini Nairobi kulipuliwa na
bomu lilokua ndani ya gari hilo.Mkuu wa polisi kituo cha pangani anasema
gari hilo lilisimamishwa na maafisa wa polisi waliolishuku kwa sababu
lilikua likiendeshwa kwenye upande wa kulia wa barabara badala ya
kushoto.Maafisa wawili wa polisi waliingia kwenye Gari hilo na
kuliongoza hadi kituo cha polisi cha pangani na baadaye bomu lilokua
ndani ya gari hilo kulipuka katika eneo la kuegeshea magari katika
kituoni humo na kuwaua watu wanne wakiwemo washukiwa wawili.
Walioshudia wanasema magari mawili
yaliokua yakifatana kabla ya lile lilokua mbele kulipuka ndani ya kituo
cha polisi cha Pangani ambapo bosco Mugendi mmiliki wa kibanda cha kuuza
bidhaa eneo la pangani alinukuliwa na BBC akisema ‘kile kilichonikuta
katika kibanda changu ni nyama ya watu iliyonirukia halafu mimi
nikatoroka na kutoka nje’

إرسال تعليق