Msanii mkongwe wa muziki nchini Judith Mbimbo maarufu kama Lady
Jaydee ameshiriki kuimba wimbo maalum wa kombe la dunia 2014
akishirikiana na David Correy na rapper wa Kenya, Octopizzo
Katika wimbo huo, Lady Jaydee na Correy wameimba kwa lugha ya Kiingereza huku Octopizzo ‘akichana’ kwa Kiswahili.
Wimbo huo ulipigwa kwa mara ya kwanza wiki hii jijini Dar es Salaam
wakati kampuni ya Coca-Cola ilipozindua promosheni yake mpya ya miezi
miwili ya Kombe la FIFA la Dunia 2014 ambayo itawawezesha wateja wake
kujishindia zawadi mbalimbali zikiwamo tiketi za kwenda kushuhudia mechi
za robo fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.
إرسال تعليق