![]() |
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency ambao ndio waandaaji wa shindano la Redds Miss Tanzania, Hashim Lundenga akiwa na Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa |
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, ambao ni
waandaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga amedai kuwa wasichana wengi
wanaoingia kwenye mashindano ya Miss Tanzania hufanya mbinu za
kuwalaghai baadhi ya watu kwenye kamati kwa kuwapa rushwa ya ngono ili
washinde taji la miss Tanzania.
Akizungumza na Global TV, Lundenga amedai kuwa kuna wasichana wanaoingia kwenye mashindano hayo wakiwa tayari kwa kila kitu.
“Kikumbwa ninachokwambia kuna wasichana ndani ya wasichana,kuna
wasichana mule ambao katika mashindano yanayokuja they are ready for
every thing,wapo wasichana hao na sisi tunajua hivyo,wasichana wanakuja
pale wameshajua mimi nimegombana na boyfriend wangu nimemuacha boyfriend
wangu kanikataza,mama yangu, baba yangu nimekuja kwajili hiyo, nilazima
nishinde, sasa anashindaje? Lazima apitepite kwa viongozi
sisi,wanapitapita sana,wanajilegeza sana kwetu sisi,sasa sisi kama
hatuna ethics ndiyo tunaingia kwenye mtego mbaya,kwasababu kuna mtu
kwenye kamati yetu tumeshamsuspend mara mbili,tunamsuspend kwasababu ya
upumbavu wake, mara mbili tumeshamsimamisha kwasababu ya upumbavu
wake,” alisema.
Kuhusu tuhuma za kuwauza warembo watu wenye pesa, Lundenga alisema: Unajua
hapa mjini, mimi leo siwezi kusema Musofe simjui,siwezi sema mapedejee
gani simjui, najuananao ndio watu wa mjini hao,tunakula nao tunalala
nao, si ndio! Sasa huwezi sema completely ukaknock-out, haiwezekani,no
it’s very difficult, akina nani wote wa Musoma yule,akina nani, huwezi,
hao ndio mapedejee wa mjini.”
إرسال تعليق